Habari za Punde

MKAKATI WA KUBORESHA AFYA ZA WATOTO MASKULINI WAANDALIWA

Wataalamu wa elimu ya afya ya Jamii kutoka Wales nchini Uingereza wameandaa mkakati wa kuwasaidia watoto nchini ya Zanzibar.

Lynne Perry, ambae ni mkuu wa kitengo cha afya ya jamii katika mji Pembrokeshire, karibuni alifanya ziara katika visiwa vya Zanzibar ili kuandaa mikakati ya maandalizi ya mradi huu ambao utaanzia katika Wilaya ya Kaskazini A. Katika kisiwa cha Unguja.

Lynne Perry alisema kwamba katika muda wa wiki mbili alizokuwepo Zanzibar, alikutana na wadau wa sekta mbali mbali wakiwemo Wakurugenzi, Makatibu Wakuu wa wizara za Afya, Elimu pamoja na KIlimo, Viongozi wa asasi zinazojitegemea, masheha na Mkurugenzi wa British Council.

“Tumeweza kuainisha baadhi ya maeneo katika maskuli yanayohusiana na sekta ya afya ambayo yanaweza kuboreshwa kwa kuanzishwa kwa programu kama zilizoanzishwa Wales” Alisema Lynne.

Ingawa mazingira tofauti ila kuna vitu vinaweza kufanyika kwani katika baadhi ya maskuli kuna vyoo viwili tu na mfereji mmoja kwa wanafunzi wanaofikia elfu moja . Na katika nyumba nyengine hakuna mifereji na hivyo kupata taabu katika kutafuta maji na baadhi kuyapta kwa kuyanunua.

Mradi huu ambao ulibuniwa na Sazani Associates ya Wales ambayo ni Jumiya ya khiyari inayofanya utafiti katika sekta ya mendeleo ya jamii na kudhaminiwa na British Council pamoja na THET Partnership with Global Health ambayo ilimuomba Lynne kutembelea Zanzibar ili kuweza kujionea hali halisi na vipi itaweza kuchangia katika sekta hii ya afya kwa jamii.

Chanzo. walesonline.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.