Habari za Punde

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT),Emmanuel Mpawe Tutuba amezindua rasmi tawi la Kampuni ya VISA iliyotambulika kama "Visa Day" ambapo ofisi imefunguliwa nchini Tanzania katika eneo la Masaki Jijini Dar es Salaam.Hayo yamebainishwa Leo Julai 16,2025 Jijini Dar es Salaam na Gavana wa BoT,Emmanuel Tutuba ameeleza kuwa ofisi hizo ziko Tanzania lakini itafanya kazi na nchi za Burundi,Uganda na Rwanda.Aidha ,amesema kwamba katika kipindi Cha mwaka wa fedha 2025/26 kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaotumia miamala ya kifedha ya kidijitali imeongezeka zaidi ya milioni 500 ukilinganisha na kipindi na kipindi cha nyuma.Pia amesema kuwa zamani watu walikua wanafanya miamala kwa cash,lakini kwa Sasa tips gharama zake zipo chini na tips zimeunganisha makampuni yote ya simu,kwahiyo tumeweza kuwarahisishia watu waliofanya miamala zaidi ya milioni 500 kwa mwaka,wakati huu watu wanapungua kwenye matumizi ya hundi na matumizi ya miamala kati ya benki Moja na nyingine yanaendelea kuongezeka Tutuba amesisitiza kuwa kwa sasa wanazipingeza Taasisi za malipo, kwa kuongea thamani na ubunifu Katia malipo, pamoja na kuhamasisha watumiaji wa huduma ikiwemo VIZA Kuendelea kutumia huduma zao.Sambamba na hayo Gavana Tutuba amesema kampuni za simu zimekuwa na utaratibu mzuri wa kufuata miongozo inayotolewa na Benki kuu ikiwemo Kuondoa na kupunguza makato yatokanayo na huduma za kulipa na kutuma pesaNaye Meneja Mkuu wa Visa nchini, Victor Makere amesema kwamba kuhusu suala la ulinzi wa kifedha wanamfumo maalum wakuhakikisha malipo yanafanyika kiusalama kwani mfumo huo endapo mteja atakosea atakuwa na uhakika wakupata fedha zake.Katika hatua nyingine Makele amesema wao kama kampuni wanauzoefu wa muda mrefu hivyo kitendo cha wao kufungua ofisi tanzanian kunatokana na kujiridhisha kuhusu faida zitakazo patikana kwenye mnyororo wa thamani kwani wamelenga soko kubwa lililopo kwenye nchi Wanachama wa jumuiya ya Africa mashariki kwa ujumla amesema makele

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.