Habari za Punde

DK. SHEIN AZINDUWA KIKAO CHA NANE CHA BARAZA LA WAWAKIILISHI.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein akitoka katika ukumbi wa Baraza baada ya kulizinduwa rasmin baraza la 8 akiongozana  na Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na Makamo wa Kwanza wa Rais Seif Sharif Hamad.  

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali, kushoto Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, Makamo wa Pili wa Rais wa ZANZIBAR Balozi Seif Ali Iddi, kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Hamid Mahmoud na  Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Sharif Hamad. wakiwa nje ya ukumbi wa BARAZA LA WAWAKILISHI baada ya kulizindua leo.     

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na Jaji Mkuu wa Zanzibar Hamid Mahmoud wakizungumza nje ya jengo la Baraza baada ya kuzinduliwa Baraza hilo la Kikao cha 8 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
Makamo wa kwanza wa Rais  Maalim Seif Sharif Hamad akilakiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Hamid Mahmoud wakati alipowasili katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi leo.  Kulia kwa Jaji mwenye Joho ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.