Habari za Punde

KUAPISHWA SPIKA NA WAJUMBE WAPYA WA BARAZA LA WAWAKILISHI

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wa CUF wakisuhudiwa wajumbea wenzao wakila kiapo cha kutumikia Wananchi  
 

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akiendesha shughuli za Baraza baada ya kuapishwa.

SPIKA Mteule akila kiapo cha utii cha kuliongoza Baraza la Wawakilishi baada ya kuchaguliwa kwa kura nyingi kumshinda mpizani wake wa CUF Abass  Muhunzi, katikati Katibu wa Baraza Ibrahim Mzee.    
MUWAKILISHI wa Kwamtipura CCM Hamza Hassan, katikati Hija Hassan wa Kiwani CUF na Omar Ali wa CUF Chakechake wakipongezana kwa kuweza kutetea nafasi zao na kurudi baraza tena kwa kipindi kingine.     
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi kulia Muwakilishi wa Mkwajuni Mbarouk Mtando na wa Donge Ali Juma Shamuhuna wakibadilishana  mawazo ndani ya baraza wakisubiri matokeo ya kura ya SPIKA  wa Baraza.   
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi wakisimama wakati ukiimbwa wimbo wa Taifa la ZANZIBAR ili kuanza shughuli za Baraza
MFANYAKAZI  wa Baraza la Wawakilishi akigawa Kura za kumchaguwa Spika wa Baraza kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi leo
MFANYAKAZI wa Baraza akipita kukusanya kura za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi baada y kupiga kura zao
MUWAKILISHI  wa Chonga CUF Abdalla Juma Abdalla  akiapa mbele ya Katibu wa Baraza.   
WAWAKILISHI wa CUF wakipongezana baada ya kurudi mjengoni kwa kipindi kingine, wakati wa kikao cha kumchaguwa Spika na Kuapishwa Wajumbe wa Baraza. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.