Kituko cha kufungia mwaka
Katika kituko kilichonisikitisha cha kufungia mwaka niliposikia kwamba kwenye uchaguzi wa ZFA Mwenyekiti aliyedumu kwa miaka 22 Ali Fereji Tamim, amechaguliwa tena kuiongoza ZFA kwa miaka mine mengine baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu Suleiman Mahmoud Jabir. Tamim alipata kura 32, Jabir kura 20 na Munir Zakaria 2.
Nimekiita kituko kwa sababu jamii ya viongozi wa soka Zanzibar wameonesha na kutujuulisha na kutwambia kwamba hawataki mabadiliko na ima wanaridhishwa na uongozi wa Soka uliopo au hawakuridhishwa na uwezo wa viongozi mbadala waliojitokeza.
Binafsi sina matatizo na Ali Ferej Tamim ila sioni mantiki ya kuendelea na kiongozi aliyedumu katika Uongozi kwa miaka 22 kwamba bado tunamuhitaji na hali halisi ya spidi ya maendeleo ya mchezo wenyewe kwa sisi tuliocheza na tunaopendelea mchezo huu tunaiona. Huna haja hata ya kuambiwa.
Siamini kwamba hii ndiyo sababu lakini sababu hasa imefichwa ndani ya pazia licha ya kusisitizwa kutumika rushwa ya hali ya juu na bila ya kukamatwa mtu yeyote na licha ya tishio la mgombea kiti cha Umakamo Aman Ibrahim Makungu ambae alitamka hadharani kwamba hatokuwa tayari kufanya kazi na Tamim pindipo akichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti.
Makungu aliondoka kabla ya kutangazwa matokeo na tunasubiri msimamo wake kwani viongozi wenzake tayari walimchagua huyo ambaye yeye alimkataa na yeye kuchaguliwa kama Makamo Mwenyekiti.
Jibu la matatizo ya Soka Zanzibar sasa limeshapatikana kumbe ni viongozi wenyewe wa soka. Kila siku tulikuwa tukitafuta mchawi na kidudu mtu, uchaguzi umetuonesha bayana.
Pongezi viongozi wa Soka Zanzibar kwa kuendeleza kulididimiza soka la nchi yetu. Hongera.
No comments:
Post a Comment