Habari za Punde

KUTOKA BARAZANI: SERIKALI INA LENGO LA KUIMARISHA UCHUMI - HAROUN

WAZIRI waNchi Uwezeshaji wananchi kiuchumi Haroun Ali Suleiman, amesema Serikali ya awamu ya saba ina lengo la kuhakikisha shughuli za wananchi za kiuchumi katika majimbo yote ya Zanzibar zinaleta tija pamoja na kipato chao kinanyanyuka na kuweza kumudu maisha yao ya kila siku.

Alisema Serikali inalengo la kufanya hivyo ili kuhakikisha shughuli za wananchi za kiuchumi zinaleta tija, kipato chao kinaongezeka na kila mwananchi anakuwa na maisha bora.

Alisema miongoni mwa mipango ambayo imepangwa kusimamia utekelezaji wa sera ya ajira na program ya kazi ambazo kwa pamoja zinalengo katika kukuza fursa za ajira rasmi na zisizorasmi kwa lengo la kukuza kipato na kuimarisha hali ya ,maisha kwa wnanchi.

Hayo alisema jana alipokuwa akijibu swali la Salmin Awadh Salmin (Magomeni) aliyeuliza Serikali hii mpya yenye muundo wa umoja wa kitaifa inamipango ipi mizuri ya kuhakikisha wananchi wa majimbo yote ya Zanzibar bila ya ubaguzi wanafaidika na mipango ya Seerikali yao pindi ilipoanzishwa.

Aidha alisema serikali kupitaiwizara yake inampango wa kuwaondoshea bughudha wananchi katika kuipata fursa ya kupokea mikopo ya JK kwa wakati.

Alisema mikopo hiyo ilizuiliwa kutolewa kwa wanchi kutokana na tatizo la ucheleweshaji wa kurudisha mikopo hiyo jambo ambalo lilifanya mzunguko wa fedha kutokwenda kwa wakati.

Waziri Haroun aliyasema hayo alipokuwa akijibu suala la nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh alipotaka kujua Wizara inampango gani wa kuyafufua matumaini ya wananchi kupata mkopo wa JK

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.