Habari za Punde

KUTOKA BARAZANI: ENEO LA KOJANI KUWA HIFADHI YA TAIFA - MBAROUK

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imesema inaandaa mipango ya kuanzisha hifadhi ya eneo la Kojani ili kuendeleza uhifadhi wa mazingira ya bahari.

Hayo aliyasema Waziri wa Mifugo na Uvuvi Said Ali Mbarouk wakati akijibu suala la Hassan Hamad omar mwakilishi wa Kojani aliyetaka kujua iwapo kuna mikakati yoyote ya uhifadhi wa Mazingira kwa wavuvi wa maeneo ya Kojani.

Alisema, hatua hiyo imechukuliwa kutokana na mwamko mkubwa wa wavuvi wa eneo hilo katika kuendeleza uhifadhi wa mazingira ya bahari hiyo .

Aidha alibainisha kuwa hatua ya uanzishaji wa hifadhi hiyo itaanza mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo baina ya wananchi wa eneo hilo na Wizara yake.

Katika hatua za kuwaendeleza wavuvi wa eneo hilo, alisema Wizara tayari imechukua hatua za kuwabadilishia nyavu ambapo kwa upande wa Tumbe nyavu 25, Kojani 5, Mkoani 8, Kizimkazi 18 na Chukwani nyavu 17 zilitolewa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.