WIZARA ya miundombinu na Mawasiliano kupitia shirika la meli imesema, imeandaa mpango wa kuziuza meli zake zilizopo sasa na kwa lengo la kununua meli nyengine mpya na za kisasa.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Miundombinu na mawasiliano Ussi aliyasema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Mfenesini Ali Abdullah Ali alipotaka kujua iwapo kunampango wa kuiuza meli ya MV. Maendeleo kutokana na uchakavu unaoikabili.
Alisema, uamuzi wa kuiuza meli hiyo kwa sasa hauwezekani kuchukuliwa hadi hapo serikali itkaponunua meli nyengne ya kuweza kuwahudumia wananchi wa Unguja na Pemba.
Aidha alisema serikali imeahirisha mpango wa utengenezaji wa meli mpya nchini Afrika kusini kutokana na gharama kubwa ambapo kwa sasa wanatafuta sehemu itakayoweza kutengeneza kwa gharama nafuu.
Alisema serikali imepanga kutafuta meli za gharama nafuu ambazo ni za kisasa zaidi zitakazoweza kutoa huduma kwa kwenda na wakati.
No comments:
Post a Comment