JUMLA ya wagonjwa 119 wenye maradhi ya figo wametibiwa Hospitali ya Mnazi mmoja kwa kipindi cha mwaka 2009/2010.
Hayo yameelezwa na Naibu wa Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk Sira Ubwa alipokuwa akijibu swali la Salmin Awadh Salmin (Magomeni) aliyetaka kujua kuna wagonjwa wangapi waliofanyiwa upasuaji na kuingizwa figo jengine pamoja na wale ambao wanaendelea kutumia dawa .
Alisema wagonjwa watatu walifanyiwa upasuaji wa kuwekewa figo Nchini India kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii na inawezekana kuna wengine walifanyiwa uwekaji figo kwa gharama zao.
Alifahamisha kuwa wastani wagharama z adawa kwa mgonjwa mmoja ni shilingi Millioni thelathini kwa mwaka na inawezekana kubadilika kulingana na idadi yaaina ya dawa zitakazohitajika.
Aidha alisema Serikali inampango wa kuanzisha kitengo cha figo kutokana na kuwa Hospitali ya Mnazi mmoja inatakiwa kuwa ya rufaa.
Hayo aliyasema alipokuwa akijibu swali la Omar Ali Shehe aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuanzisha kitengo cha figo katika Hospitali ya Mnazi mmoja
No comments:
Post a Comment