Na Sheikha Haji Dau na Halima Abdalla
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Fatma Abdul Habib Ferej amesema Wizara yake ikishirikiana Taasisi mbali mbali kulipatia ufumbuzi tatizo la uchimbaji mchanga katika eneo la mwanakwerekwe makaburini linaondoka.
Alisema Tarehe 20 /12/2010 Ofisi ya makamo wa kwanza ilikutana na wadau kutoka Wizara ya Kilimo na Maliasili,Jeshi la polisi ,Ofisi ya Kadhi Mkuu,Mufti Mkuu ,Kamisheni ya Wakfu ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
Waziri Ferej aliyasema hayo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu swali la Salmin Awadh Salmin(Magomeni) aliyetaka kujua Serikali ime imechukua hatua vipi katika kukabiliana na vitendo hivyo .
Waziri alisema mikakati iliyoekwa katika kikao hicho ni pamoja na kulitambua eneo hilo pamoja na kulijengea eneo hilo kwa kulizungushia ukuta ikiwa ni pamoja na kuzibomoa nyumba ambazo zimejengwandani ya eneo hilo pamoja na kueleimisha jamii ubaya wa vitendo hivyo.
Aidha alisema Serilali imeona kuna tatizo katika eneo hilo hivyo kuna haja ya kutafuta eneo jengine mbadala ambalo litasaidia kwa ajili ya kuzikia.
Hayo aliyasema alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mahmoud(Kikwajuni) aliyeuliza Serikali inampango gani wa kutafuta eneo jengine kwa ajili ya kuzikia kwa vileeneo la Mwanakwerekwe limejaa.
No comments:
Post a Comment