Habari za Punde

SAIDIA ELIMU ZANZIBAR - BADO MISAADA INAHITAJIKA KUSAFIRISHA VIFAA KUTOKA MAREKANI KWENDA ZANZIBAR


Napenda kuchukua nafasi hii adhimu mbele yenu kuufikisha ujumbe huu wa kheri kwenu.

Kwa niaba yangu binafsi, Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla waliopo hapa Washington State nchini Marekani, tunapenda kutumia nafasi hii kutoa maelezo ya vifaa vilivyopo hivi sasa katika Storage zetu kwa hatua ya usafiri kutoka Bandari ya Seattle, Marekani hadi Zanzibar.

Vifaa hivi vimekusanywa kutoka kwa wafadhili mbali mbali waliojitolea kwa ajili ya kusaidia juhudi za maendeleo huko Zanzibar, Tanzania.

Vifaa vyenyewe ni meza, Computers, wheel chairs, roundtables, books shelves, books na kadhalika.

Vifaa hivyi ni mchango wa Wazanzibari na Watanzania katika kusaidia juhudi za kuondoa kero mbali mbali zinazowakabili jamii yetu huko nyumbani katika huduma za Elimu kama ukosefu wa vitabu katika Maktaba, vifaa vya kukalia katika Maktaba, huduma za computer bado ni ngumu kupatikana ipasavyo katika mashule mbali mbali pamoja na Maktaba Kuu mpya iliyopo huko Zanzibar na Hospitali nyingi kukosa huduma za vifaa kama wheels chairs na kwa matumizi ya Walemavu kwa ujumla.

Napenda kutumia fura hii kama changamoto kuwaomba ndugu zangu kutoka Tanzania na Zanzibar kwa ujumla hususan waliopo nje kwa nia njema kuchangia kwa hali na mali misaada ya kifedha kwa ajili ya usafirishaji wa vifaa vyote viliopo sasa kutoka Seattle hadi Zanzibar mwezi Jan 2011. Ndugu zenu tayari wamefanya kazi kubwa katika kutafuta wafadhili na hatimae kufanikiwa kukusanya vifaa vilivyotajwa na msaada wenu utahitajika katika kuchangia gharama za usafiri tu.

Gharama za container futi 40 ni dollars 6,500 bei hii imetokana na utafiti tuliofanya kupitia shirika la meli la Delma shipping line. Michango yote inakaribishwa kwa wote kwa kiwango cha aina yoyote na kutumwa katika account zifuatavyo

(1) NEWDAYAFRICA NON PROFIT ORGANIZATION

31217 ne 110 th St Carnation wa 98014 USA

http://www.newdayafrica.org tumia link hii kwa kutoa mchango wako kupitia online au Andika cheque kwa jina Newdayafrica/Zanzibar library project

Jumuia hii inafanya kazi pamoja katika kukusanya michango kama mfadhili wa vifaa vyetu vilivyopo.

(2) BANK OF AMERICA WA ACCOUNT NO 32000473 NAME AMIN IBRAHIM ALLY



13932 Ne 14 Th Street Apt 8 Bellevue Wa 98005 USA. Simu 01 425 943 -0074

Napenda kutanguliza shukrani nyingi na dhati kwa Raia wema wa Tanzania na Zanzibar katika kufanikisha michago yenu bila shaka kila mmoja ana dhamira kubwa katika kutoa mchango wake katika kusaidia huduma za kijamii na kuboresha hali ya maisha kwa vizazi vipya.

Tumia fursa hii kusaidia nchi yako wakati ndio huu ambapo Zanzibar inahitaji maendeleo makubwa kutoka kwa raia wake waliopo nje(Diaspora).

Kama kuna ufafanuzi wowote unaohitajika unaweza kuwasiliana nami kwa Amin_ally@hotmail.com , Simu No 01 425 943 -0074.

Ahsanteni sana.

AMIN ALLY

Washington State, Marekani, USA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.