Na Mwanajuma Abdi
SHIRIKA la Posta, limesema wanafunzi kutokujua kutumia huduma ya mtandao wa ‘Internet’ kunasababisha msongomano mkubwa wa uchukuaji wa fomu za kufanya mitihani wa kidato cha nne.
Akizungumza na Gazeti hili jana huko Kijangwani mjini hapa, Meneja Msaidizi wa Shirika hilo, Peter Mathias Bihume alisema kutokujua kutumia Interneti kunasababisha msongamano wanafunzi wengi wanaotaka kuchukua fomu hizo.
Alisema fomu za mitihani za kidato cha IV kwa vijana wanaotaka kurejea kufanya mwishoni mwa mwaka huu zinapatikana katika kompyuta, ambapo kama mtu anajua anaweza kuprinti mwenyewe na baadae kukamilisha taratibu nyengine za kutafuta kituo na hatimae kwenda Posta kwa ajili ya umaliziaji taratibu nyengine na malipo ya shilingi 40,000 gharama za mitihani na usafirishaji.
Alieleza wastani wanafunzi wanaofika hapo kwenda kuchukuwa fomu kwa siku ni 200 hadi 300 hivyo inakuwa vigumu kuweza kuwahudumia kwa haraka.
Alifahamisha kuwa, kwa siku ya kwanza walipata tabu kuwahudumia wanafunzi hao, hali iliyofanya mwanafunzi mmoja kuchukua zaidi ya dakika 10 au zaidi kwa ajili ya kumjazisha fomu, ambapo pia baadhi yao walisahau kumbukumbu za namba za mitihani waliyoifanya huko nyuma.
Meneja Msaidizi huyo alitoa wito kwa vijana kujifunza kompyuta kwani ndio njia pekee inayosaidia kurahisisha mawasiliano hususani katika wakati huu wa sayansi na teknolojia.
Hata hivyo, alisema uchukuaji na urejeshaji wa fomu huo zoezi lake litakamilika Februari 28 mwaka huu, ambapo mwanafunzi atayechelewa atapigwa faini na NECTA baada ya kulipia shilingi 40,000 atalazimika kulipia shilingi 60,000.
Poleni ndugu zngu wa zenji, tuweni makini na sayansi na teknolojia, binafsi nilijifunza intanet nikiwa darasa la nane mwaka 2001 tulikua wachache darasani wenye mail inasikitisha kuona mwanafunzi wa kidato cha nne na sita hata kushika mouse hujui, kwlei tutafika?
ReplyDeleteOsmania Hyderabad.