Habari za Punde

AJALI GARI YA KUCHUKULIA MAJI SAFI.


GARI ya kubebea Maji likiwa limepata ajali likiwa katika kazi zake za kusambaza maji  kwa wateja wao, katika barabara ya Michezani na makutano na Gymkhana. Chanzo cha ajali hiyo kinasemekana ni watoto waliokuwa katika mchezo wao wa kuinuwa ringi moja juu wakiendesha baskeli. Hakuna mtu aliyekufa katika ajali hiyo iliotokea jana usiku.   

WANANCHI  wakiangali ajali  iliotokea maeneo ya makutano ya barabara ya Michezani na Gymkhana, ajali hiyo kwa mujibu wa mashuhuda dereva wa gari hiyo la kubebea maji lenye namba za usajili Z 547 BL alimkwepa mtoto akiendesha baskeli huku akitembea na ringi moja imekuwa ni mchezo wa kawaida kwa watoto kufanya michezo hiyo barabarani bila ya kujali madhara ya ajali kwao na kwa watu wengine wanaotumia barabara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.