Hivi majuzi tumesikia uteuzi wako wa Makatibu Wakuu ambao ni watendaji muhimu wa Serikali. Kabla ya hapo tulikusikia ukituteulia Wakurugenzi kukamilisha safu ya Utendaji serikalini.
Ila kuna uteuzi ambao ni wewe pekee mwenye uwezo wa kuufanya kikatiba ila bado hatujakusikia kwani hata Rais aliyepita naye pia hakufanya. Uteuzi wa Kadhi Mkuu na Mufti Mkuu.
Tokea kufariki kwa Kadhi Mkuu Ali Khatib Mranzi, Allah Subhaanahu Wata’ala amrehemu, hadi hii leo si Rais aliyepita wala wewe hatujakusikia bado kututeulia kiongozi muhimu katika upande wa Serikali kuhusiana na mambo ya Dini.
Tokea kututoka kwa Mufti Mkuu Zanzibar ‘Allaamah Haarith bin Khelef, Allah Subhaanahu Wata’ala, amrehemu hadi hii leo hatujasikia kuteuliwa kwa Mufti mwengine.
Angalau kuna Naibu Kadhi Mkuu kwa hivyo kitengo hiki kinaweza kufanya kazi lakini hatuna Naibu Mufti Mkuu. Ila tutaendelea kwa miaka mingapi kukaimiwa na cheo hiki Muhimu cha Kadhi wakati tuna Rais aliye madarakani na tunamsikia akifanya uteuzi wa vitengo vingi vya Serikali.
Mheshimiwa Rais litupie macho suala hili kwani sijui vigezo gani hutumika katika kuwateua Waislamu wenye sifa za kuweza kuwa Kadhi na Mufti Mkuu lakini niaamini kwa busara zako utalishughulukia.
Washukran
MAKAMU WA RAIS AZITAKA TAASISI ZA FEDHA KUFUATA NYAYO ZA CRDB BENKI.
-
Na.Ashura Mohamed -Arusha
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdory Mpango
amezitaka Taasisi nyingine za fedha nchini kuendelea ...
9 hours ago
Huu ni kudhalilika kwa Waislamu. Inakuwaje ategemewe raisi kufanya uteuzi wa mufti. Hii si inaonesha kuwa serikali ina mkono katika masuala ya dini? Inakuwaje wakristo wanateua viongozi wao wenyewe lakini Waislamu bado wanamsubiri raisi. Sijui itakuwaje Zanzibar tutakapopata raisi ambae ni mkiristo.
ReplyDeleteWaislamu tukaeni chini tuchagua Mufti wetu baadae tuipe taarifa serikali.Hiyo ndio demokrasia ya kweli.
kwakumbusha tu pia kati mtendaji wakfu na mali ya amana hajachaguliwa kwa kipindi kirefu tokea afariki aliekuwepo.
ReplyDeleteAhsante mdau kwa kumuongeza Katibu Mtendaji wa Wakfu na Mali ya Amana ambye pia anakaimiwa.
ReplyDeleteNukta ya mchangiaji wa kwanza ina mantiki ni kitu ambacho ingawa leo kinaonekana hakiwezekani lakini ni suala ambalo ni Waislamu wenyewe wanapaswa kulizungumzia kwa upana faida na hasara ya kuchaguliwa Mufti, Kadhi na Serikali na kama kuna fikra mbadala ambapo kama sikosei katika miaka ya themanini iliwahi kuja fikra ya Mufti wa Waislamu wenyewe na ikapitishwa misikiti yote ya Ijumaa na kwa bahati mbaya tukasikia dhana hii pia imetekwa na serikali