Na Kauthar Abdalla
WANAFUNZI wa skuli ya Sekondari Uroa wanalalamikia upungufu wa walimu wa sayansi na ukosefu wa vifaa vya maabara hali ambayo inawafanya kutosoma kwa ari na ufanisi.
Wakizungumza na mwandishi wa habari, wanafunzi hao walisema kukosekana kwa walimu wa sayansi pamoja na vifaa vya maabara kunachangia kurejesha nyuma kiwango cha elimu kijijini hapo.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Haji Muhammed Suleimani,alisema hivi sasa wana mwalimu mmoja wa somo la Biology ambaye anatakiwa asomeshe madarasa nane kwa siku hali ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu wanafunzi pamoja mwalimu mwenyewe.
Nae Kaimu Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo, Hamid Ussi Mnemo, amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambapo alisema tayari ameshalifikisha wizarani lakini bado halijapatiwa ufumbuzi kutokana na wizara kusema hakuna walimu wa sayansi.
No comments:
Post a Comment