UZOEFU unaonesha mambo mengi yafanywayo na wazee vijana hupingana nayo. Kwa sababu kadhaa zikiwemo na kwenda na wakati.
Wazee walijuwa umuhimu wa utumiaji wa tumbaku na kuwasaidia kuimarisha afya zao na kuishi bila kutetereka.Tumeambiwa kwamba starehe ya utumiaji wa tumbaku (Ugoro) hutumika sana na wazee
katika maeneo haya ya Afrika ya Mashariki.
Uraibu huo uko tafauti na matumizi ya tumbaku ya sigireti (Sigara) ambayo hutumiwa na kila rika katika jamii wakiwemo wanawake na wanaume.
Msimulizi wa makala haya alizungumza na baadhi ya watumiaji wa tumbaku hiyo asilia na kuelezwa kuwa ndani ya ugoro mnapatikana kitu dawa na sio starehe ya moja kwa moja kama wengine wanavyofikiria.
“Kuna namna nyingi ya matumizi ya tumbaku wengine hunusa na wengine huvuta na kila moja ina faida yake katika utumiaji huo” alisema Mzee Amir wakati akisimulia matumizi ya tumbaku.
Wengine walidiriki kusema kuwa tumbaku huchapuzwa na vibwagizo vya tambuu, chokaa ikiwemo na popoo ili kuongeza ukali na uchangafu wa kinywa pia kujenga misuli pale inapotumika.
Zanzibar, jamii ya Kiswahili na ya kihindi imeonekana kuitumia sana tumbaku lakini ukweli unabaki palepale wengi watumiaji hao ni wazee.Tumbaku kwa wale wanaoitumia wanasema husaidia kuimarisha afya ya meno yao na wanaouinusa husema inakimbiza matatizo ya kamasi hayo ni kwa mujibu ya wale wanaoitumia.
Kwa upande wa vijana walipoulizwa, walisema tumbaku hata kama itakuwa ni dawa ya kuimarisha meno na kuwa tiba kwa jambo lolote lakini kwa wao ni vigumu kuitumia kwa sababu inachakaza haiba ya meno.
“Meno yanapoteza rangi yake kaka iwapo utavuta tumbaku, mimi siwafiki kuiingiza kinywani mwangu na hata puani” alisema Suweid said, wakati akichangia hoja ya utumiaji ugoro.
Hata hivyo mbali na utumiaji wa tumbaku kwa kunusa na kuvata pia wazee wengine huitumia kupaka kama wanja na kuwasaidia kuimarisha uoni mzuri wa macho ingawa msemaji wa hayo hakuweza kuthibitisha kutoka kwa ushauri wa kidakitari.
Tukiondoka katika utmiaji huo wa tumbaku kuna mambo mengi yanayofanywa na wazee hata kama yanakuwa na tija bado vijana huwa hawapendi kuyafanya na kuwekwa katika dhana ya uzee uzee.
Kwa mfano ulio wazi hapo nyuma katika Visiwa vya Unguja katika maeneo kadhaa kulikuweko vyano vya saruji na wafuaji wengi wa kujiajiri walipatikana katika maeneo hayo lakini asilimia kubwa ilikuwa ni wazee na sio vijana.
Maeneo kama Kariakoo (Kwahani), Muembe ladu (Miti ulaya), Kikwajuni (Weles) na Saateni kulikuwepo vyano hivyo na kazi za ufuaji wa nguo zilifanyika humo mpaka katika miaka ya mwishoni mwa Themanini
yalipoanza kupotea kidogo kidogo.
Leo hakuna kijana anaediriki kutaka kujiari kupitia kazi hiyo kwa maana waliokuwa wakiifanya wakati huo ni watu wazima kwa tafsiri ya wazee.
Aidha wazee waliokuwa wakifanya biashara ya kuni, kulikuwepo watu maalumu wakilipwa kwa kuchanja kuni na maisha yao yalikwenda kwa namna hizo lakini walikuwa ni wazee, sasa hali hiyo haipo tena. hakuna
kijana mwenye hamu ya kujituma kwa njia hizo.
Utamaduni wa kupiga chenga desturi zilizokuwa zikitumiwa na wazee hasa katika taratibu za kujituma wakati mwengine hukwamisha mipango ya kujipatia fedha halali kupitia nguvu zake mwenyewe kijana na kubaki
kutunduwaa vijiweni kwa maongezi na kupoteza muda.
Zipo baadhi ya kazi ambazo nazo zilifanywa na wazee kwa siku za nyuma hivi sasa kwa mbali huonekana vijana kujitumbukiza na kupata tija ingawa si kubwa lakini hukuna kupata kudogo.
Kazi hiyo ni ile ya uuzaji wa samaki iwe sokoni au kwa kutembeza vijana huifanuya kazi hiyo na kuwasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku.
Hizo ndizo kazi asili si kila mmoja ataweza kuajiriwa na Serikali, ipo haja ya wengine kubuni njia kupitia kazi za kiasili ili kuweza kuendesha maisha ya kila siku kwa mtu mmoja mmoja.
Wazee wanawake waliutumia mtama kwa kazi ya kuutwanga na kutengeneza togwa kilikuwa ni kinywaji safi chenye kujenga mwili kutokana na nafaka inayotumika kwa kupata ulaji huo.
Uji wa kunde, mtama, ngano nzima si lazima vifanywe na wazee vijana wanao uwezo wa kufanya hayo na kujipatia fedha halali na kuwa ndio chanzo cha kujituma.
Jamii ya kileo inatakiwa kukumbuka na kuziendeleza shughuli asilia bila kujali nani waliokuwa wakizifanya kazi hizo kwa maana ya kuingia katika zama za uhuishaji wa mambo ya kiasili kupitia vijana na sio wazee ambao leo nguvu zao zinakwisha na baada ya muda wataondoka bila ya kupata wa kuwarithisha.
No comments:
Post a Comment