Habari za Punde

VIJIDUDU VYA MALARIA SUGU VYANYEMELEA AFRIKA

Vijidudu vinavyoweza kuhimili dawa za kutibu Malaria ambavyo tayari vimeshaenea katika nchi za Kusini mwa Asia vinaweza kufika Afrika wakati wowote na kuwaweka wananchi wengi, hasa watoto, katika hatari ya kuambukizwa na vijidudu hii hatari kwa mujibu wa mtaalamu wa maradhi ya tropiki, Profesa Nicholas White.

Profesa White ameomba kuharakiza kinga kuliko tiba kama mkakati wa kukabiliana na vijidudu hivi ambavyo kwanza vilianzia katika miji ya mipakani katika ya Thailand na Cambodia.
Aina hii ya Malaria huchukua muda mrefu kupona na vidonge vya kutibu kama artemisinin kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo ila kama vijidudu vitaweza kufika Afrika kuna hatari ya kuweza kuleta maafa makubwa.
Ingawa shirika la Afya la kimataifa (WHO) limejaribu kwa kiasi kikubwa kuzuia kuenea kwa vijidudu hivi kwa kuwekeza Dola Milioni 111 katika kutafiti na kubuni dawa nyengine zenye nguvu ya kuweza kukabiliana na vijidudu hivi bado kunaweza kutokea madhara makubwa.
Kwa mujibu wa Profesa White vita hivi viharakizwe katika muda  wa miezi na si miaka kama wengi walivyopanga kwani muda ndio muhimu zaidi kuliko upangaji wa muda mrefu.
Kama ambavyo ilishindwa chloroquine kutibu Malaria ndipo tunapoelekea kwa sasa kushindwa kwa artemisinin kwani ilipovumbuliwa ilihesabika ni dawa kiboko dhidi ya Malaria.
Malaria huwakumba takriban watu milioni 243 kwa mwaka na 863,000 hufariki kila mwaka kutokana na Malaria.
Sijui kwa upande wetu visiwani tutajipanga vipi endapo aina hii ya Malaria itafika na kuleta madhara makubwa huku kila siku tukiimba wimbo wa vita dhidi ya Malaria lakini bado ipo na itaendelea kuwepo. Hii ni kwa tahadhari tu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.