Habari za Punde

UZINDUZI WA TAMASHA LA WIKI YA UTAMADUNI WA OMAN MAKUMBUSHO YA TAIFA BEIT AL AJAB FORODHANI.

WASANII kutoka Oman wakicheza Ngoma yenye asili yaOman katika serehe za ufunguzi wa Tamasha la siku ya Utamaduni wa Oman  katika viwanja wa Makumbusho ya Taifa Beit Al Ajab. 
MAMBO ya Ngoma za Utamaduni wa Oman. 
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd  wa tatu kulia akiangalia ngoma katika sherehe za uzinduzi nwa tamasha,kutoka kulia Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Majid Abdalla Al Baad, Naibu Waziri Urithi na Utamaduni wa Oman Shekh. Hamad Al Mamriy, Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Abdilla Jihad Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.    
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifunguwa Tamasha ski ya Utamaduni wa Oman katika iwanja vya Makumbusho ya Taifa Forodhani Beit Al Ajab.
Balozi Mdogo  wa Oman Zanzibar Majid Abdalla Al Abaad  akitowa maelezo ya matayarisho ya Tamasha hilo wakatik wa ufunguzi wake uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. 
NAIBU Waziri wa Urithi na Utamaduni Shekh. Hamad Al Mamriy akitowa hutuba yake kwa niaba ya Wananchi wa Oman katika sherehe za kuzinduwa siku ya Utamaduni wa Oman.


WANANCHI walioalikwa katika uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Oman linalofanyika katika ukumbi wa Beit Al Ajab na Ngome Kongwe.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Ali Mwinyikai. akitowa maelezo ya ushirikiano  wa Utamaduni wa Zanzibar na Oman. 
BAADHI ya Viongozi wa Oman waliofuatana na Wasanii kuadhimisha siku ya Utamaduni Oman Zanzibar wakifuatilia uzinduzi huo.
WANANCHI wakifuatilia ngoma za Utamaduni wa Asili ya Oman
WAANDISHI wa Habari wakiwa katika harakati za kufanikisha shughuli hiyo ili kuwafikia Wananchi hawakupata fursa ya kuhughuria Tamasha hilo.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipata maelezo ya moja ya bidhaa za fedha za asili ya Oman katika maonesho hayo. 
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiangalia moja ya picha za Oman zikiwa katika maonesho hayo zinazoelezea matukio na mandhari ya Oman.  
VIONGOZI wa Serikali wakiangalia picha katika tamasha hilo.  


WANANCHI wakipata huduma ya kuandika majina yao kwa lugha ya Kiarab kutoka kwa msanii wa Oman ikiwa ni moja ya maonesho ya Utamaduni wa Oman.



WANANCHI wakipata fursa ya kuagalia picha katika tamasha hilo la siku ya Utamaduni wa Oman.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akikabidhiwa zawadi na Naibu Waziri wa Urithi na Utamaduni wa Oman Shekh. Hamad Al Mamriy  baada ya uzinduzi.   
MSANII Abdulmubarak Rabia, akionesho usanii wake wa kuchonga Jahazi katika maonesho hayo ya siku ya Tamasha la Utamaduni wa Oman. 
MAENESHO ya Mavazi ya Kioman
WASANII wakionesha jinsi ya urembo wa upakaji wa Hina ya Kioman katika tamasha hilo  wakati wa ufunguzi wake, na kutowa huduma hiyo kwa Wananchi wanaofika katika maonesho hayo bure bila ya malipo ikiwa ni kuimarisha uhusiano wa kitamaduni na Zanzibar. 
MSANII Husna Abeid akionesha jinsi ya ufumaji wa mazulia yanayotumiwa na wananchi wa Oman.
MSANII akiomnesha Utamaduni wa Oman katika kuweka mapambo ya fedha  
MAMBO ya Haluwa ya Kioman moja ya kivutio kwa Wananchi wa Zanzibar katika Maonesho hayo. 
MAANDISHI ya Kiarab yakiwa katika maandiko ya Kisanii ikiwa ni moja ya picha katika maonesho hayo.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.