Na Abdi Shamnah
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar , Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali za mitaa nchini, zinakabiliwa na kazi kubwa ya kusimamia maendeleo ya wananchi kwa kuzingatia kuwa Watanzania walio wengi ni wakulima.
Maalim Seif amesema hayo leo katika viwanja vya nane nane mjini Dodoma , alikofika kuangalia maonyesho ya wakulima, yanayokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Amesema Serikali za mitaa ndio chombo kilicho karibu zaidi na wananchi na kufahamu matatizo na kero mbali mbali zinazowakabili.
Akizungumza na Viongozi wa Mkoa huo, waandaji wa maonyesho hayo pamoja an waandishi wa habari, Maalim Seif alisema iwapo serikali hizo zitafanya kazi zake ipasavyo na kuhakikisha kila senti inayotolewa na serikali inatumika ipasavyo, ni wazi kuwa maendeleo ya haraka katika kilimo yatafikiwa.
Alisema taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali nchini, zinaonyesha kuwepo kasoro kubwa ya upotevu wa fedha unaotokana na usimamizi mbovu wa serikali za mitaa.
Aliwataka watendaji katika Serikali hizo kuondokana na ufisadi katika ununuzi wa pembejeo za kilimo na kuwaomba wananchi kuwa macho dhidi ya watu wachache wanaokwamisha maendeleo
Maalim Seif ambae katika ziara hiyo alipata fursa ya kutembelea mabanda na taasisi mbali mbali, alishauri taasisi zinazohusika kuyatangaza yale yote yanayofanyika katika kuimarisha kilimo ili Watanzania wayajue.
Alisema tayari nchi imepiga hatua kubwa na maonyesho hayo yanathibitisha jinsi
Alisema kuna umuhimu mkubwa wa mafanikio yaliokwisha kupatikana katika uimarishaji wa kilimo kutafisriwa moja kwa moja kwa wakulima.
Aidha aliishauri Serikali na taasisi zinazosimamia uingizaji wa pembejeo nchini kupunguza gharama za ununuzi ili wakulima wa kawaida waweze kuzimudu.
Katika ziara hiyo Maalim Seif alipata fursa ya kuyatembelea mabanda na taasisi mbali mbali ikiwemo, CRDB, Manispaa ya Singida,Wizara ya
No comments:
Post a Comment