Habari za Punde

WADAU WA UTALII PEMBA WATAKIWA KUSHIRIKIANA

Na Suleiman Rashid, Pemba  

AFISA Mdhamini  wa Kamishin ya utalii Pemba, Suleiman Amour Suleiman, amesema sekta ya utalii kisiwani Pemba inakabiliwa na changamoto nyingi na kuwataka wadau wa utalii kujenga umoja na mashirikiano ili kuikuza sekta hiyo kisiwani hapa.

Hayo ameyasema ukumbi wa hoteli ya Clove Inn mjini Chake Chake, alipofungua semina ya siku moja iliyowashirikisha wadau wa utalii  wapatao 50 kisiwani hapa.
 Alisema ukosefu wa  wa miundombinu maeneo  yenye vuvitio vya kitalii kama vile fukwe,  maeneo ya kihistoria kama  magofu ya kale na taaluma ndogo kwa wananchi  kuelewa juu ya dhana ya utalii na umuhimu wake  imekuwa miongoni mwa matatizo yanayoikabili sekta hiyo.
Aliwataka wadau wa utalii  kisiwani Pemba kujenga mashirikiano  umoja na maelewano ilikushinda changamoto zinazoikabili sekta hiyo kwa lengo la kunyanyua utalii kisiwani humo, uboreshe kilimo na kunyanyua uchumi wananchi na serkali iweze kupata kipato.
 Akielezea changamoto ya ukosefu wa taaluma, alisema watu wengi kisiwani hapa hudhania kuwa utalii unaoletwa na wazungu  ni mbaya, hivyo kuanza kuupinga ila inapotokeazea kukaa nao na kuwaelewesha hukubali hivyo ni dhahiri kuwa bado watu walio wengi wanauangalia utalii kwa mtazamo hasi badala ya kuuangalia katika mtazamo unaokubalika.
 Katika mafunzo hayo mada mbali mbali zilijadiliwa ikiwa pamoja na Dhima kwa mawakala wa safari, Faida za kiuchumi katika sekta ya utalii, na kazi kuu za watembeza watalii.
  Nyengine ni Changamoto zinazoikabili sekata ya utalii kisiwani Pemba ya uwepo ya miundombinu mibovu inayonyima fursa ya watalii kutembelea baadhi ya maeneo na hata watembeza watalii kutokuwa na lugha fasaha za kuwavutia watalii.
 Waliofaidika na semina hiyo ni pamoja na watembeza watalii, madereva wa magari yanayosafirisha wageni, ikiwa ni pamoja na watalii, wamiliki wa hoteli za kitalii, wafanyakazi wa hoteli za kitalii na wananchama wa jumuia ya PATI.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.