Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ameondoka nchini jana tarehe 15/09/2011 kuelekea India kwa ziara ya kikazi ya wiki mbili.
Katika ziara hiyo Maalim Seif anafuaana na mkewe Mama Awena pamoja na viongozi wengine wa Serikali akiwemo Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Bw Nassor Ahmed Mazrui.
Vionozi wengine ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Amali Bw Ramadhan Abdalla Shaaban na Katibu Mkuu Wizara ya kilimo na Maliasili Bw Afan Othman Maalim.
Baada ya ziara ya kikazi Maalim Seif anatarjiwa kufanyhiwa uchunguzi wa afya yake kufuatia operesheni ya magoti aliyofanyiwa miezi sita iliyopita Hospitali ya Appolo. Maalim Seif anatarajiwa kurudi nchini tarehe 05/10/2011.
No comments:
Post a Comment