Habari za Punde

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA MALAYSIA

Kwa niaba ya Wanafunzi wa Tanzania wote wanaoishi Malaysia .Tumeshitushwa sana na habari za tukio hili na tunaungana pamoja katika kuomboleza mtihani mkubwa huu uliotokea tareh 10/9/2011 wa kuzama kwa meli ya The MV Spice Islander na kusababisha vifo vya ndugu zetu . Katika hili hakuna wa kushukuriwa na kuombwa ila Mwenyezi Mungu kwa kuwapa uhai ndugu zetu na kuwarudisha mbele ya hali kwa wakati aliowapangia.


Msiba huu umetutia simanzi kubwa sana na tunamuomba M/Mungu atupe subra na atuzidishi umoja katika kuomboleza tulio hili la msiba a Taifa.
Tunakuombeni mtufikishie salama zetu kwa viongozi wetu tulioataja hapo chini na ndugu zetu wote huko nyumbani.

1. Mhe Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein,
2. Mhe Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na
3. Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi.

Tunaungana na ndugu zetu kuomboleza na kutia fat-ha kwa msiba huu mkubwa sana uliotutokea.
Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Aamin


Makame Hj Mohamed
Kuala Lumpur
Malaysia

3 comments:

  1. Wandugu,tunapokea kwa moyo mkunjufu rambi rambi zenu lkn,jamani mkimaliza masomo mrudi nyumbani hali bado sio shawari huku,unaweza hata ukahoji uwezo wa baadhi ya watu kufikiri na kuamua mambo,hivi inakuaje meli iliyolala ubavu kwa saa kadhaa inaachwa mpaka inazama wakati tagi zipo! tunaipongeza SMZ kwa juhudi zake lkn.bado ina mswali mengi ya kujibu...Mpeni hi mdau MWINYI TALIB kama mko naye!

    ReplyDelete
  2. sawa mkuu uciwe na shaka tutarudi kuja kuliendeleza taifa letu tukiwa sambamba na mdau wetu MWINYI TALIB

    ReplyDelete
  3. Usiwe nawasiwasi inshallah tutarudi tuje kujenga nchi yetu, ndugu yetu Idris Rai kaonesha njia. Allah amlipe kwa moyo wake

    From UPM Malaysia

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.