Habari za Punde

RAMBIRAMBI KUTOKA ZANZIBAR COLLEAGUES - MALAYSIA

Kwa niaba ya uongozi wa Zanzibar colleagues in Malaysia, tumezipokea kwa mshituko na majonzi makubwa taarifa za kuzama kwa meli ya MV spice Islander usiku wa kuamkia tarehe 10/09/2011, na kusababisha vifo vya wazanzibar wenzetu wapendwa.


Kwa niaba ya Mwenyekiti,katibu,na naibu katibu wa ZANZIBAR COLLEAGUES IN MALAYSIA,tunapenda kutoa mkono wa pole na rambirambi kwa wananchi wote wa Zanzibar pamoja na viongozi wao wote.

Rambirambi pia ziwafike Rais wa Zanzibar pamoja na serikali yote ya umoja wa kitaifa (SUK)

Rambirambi zetu ziwafike ndugu, jamaa,na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika ajali hii.Msiba huu ni wetu sote na tunamuomba mwenyezi mungu atupe moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa,bila ya kusahau kuwaombea dua wale wote waliotangulia mbele ya haki Allah awape safari njema na awape mwisho mwema.

Tunawapa pole wale wote waliookoka na tunamuomba Allah awaponeshe haraka ili warejee katika shughuli za ujenzi wa nchi.

Na mwisho kabisa,Allah (s.w) anasema,Na tutakujaribuni kwa kila jambo kutokana na khofu na njaa,na kupungukiwa na mali na nafsi na mazao,basi wabashirie wenye kusubiri na ambao inawapata misiba husema”hakika sisi ni wa M\Mungu na hakika kwake ni marejeo surat (Al-baqara)

MWENYEKITI
ZANZIBAR COLLEAGUES IN MALAYSIA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.