Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu mpya wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Khalifa Hassan Chum kuwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Balozi Hussein Said Khatib kuwa Mjumbe wa Kamisheni ya Utalii wa Umma Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Mohammed Faki Mohammed kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.
Picha zote na Hamad Hija, Maelezo
Stori na Rajab Mkasaba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi mbali mbali akiwemo Sheikh Saleh Omar Kabhi kuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Othman Masoud,Mawaziri, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdala Mwinyi, Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wengine.
Dk. Shein pia, amemuapisha Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Sheikh Hassan Othman Ngwali kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Wengine ni Bwana Muumin Khamis Kombo aliyeapishwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashataka, Zanzibar. Bwana Abdulrahman Mwinyi Jumbe Mshauri wa Rais Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Dk Shein pia, amemuapisha Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa kuwa Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa na Uwekezaji, Bwana Burhan Saadat Haji kuwa Mshauri wa Rais Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi ambapo Bwana Issa Ahmed Othman amemuapisha kuwa Mshauri wa Rais Utalii.
Aidha, Dk. Shein amemuapisha Bwana Mohammed Fakih Mohammed kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, Jaji Hamid Mahmod Hamid, Bwana Mbarouk Jabu Makame, Bwana Issa Mohammed Suleiman, Bwana Ali Rajab Juma, Balozi Hussein Said Khatib na Bwana Jecha Salim Jecha ambao wote wameapishwa kuwa Wajumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.
Wakati huo huo, Rais Dk. Shein amempandisha Cheo Bwana Khalifa Hassan Choum na kumuapisha kuwa Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment