Habari za Punde

ZANTEL YATOWA MSAADA WA MADAWA HOSPITAL YA MNAZI MMOJA KWA AJILI YA MAJERUHI WA AJALI YA MELI SPICE.

 MKURUGENZI Fedha wa Kampuni ya simu ya Zantel Zanzibar Abdul Wahid Talib akisoma salamu za kampuni yake kuhusu msada huo wa dawa wakati wakikabidhi msaada wao kwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Sira Ubwa Mwamboya, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Hospital  

 MKURUGENZI wa Fedha wa Zantel Abdul Wahid  Talib kulia akimkabidhi msaada wa dawa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Sira Ubwa Mwamboya kwa ajili ya kutowa huduma kwa Wahanga wa Meli ya Mv Spice iliotokea wiki iliopita wakati  ikiwa katikac safari yake ya kwenda Pemba.
 NAIBU Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Dk.Sira Ubwa Mwamboya akitowa shukrani kwa kampuni ya simu ya mkoni ya Zantel kwa msaada wake wa dawa ukiwa umetolewa wakati mwafaka katika kipndi hichi kugumu serikali ikikabiliwa na janga la maafa ya kuzama kwa meli ya mizigo na abiria ya MV Spice, wiki iliopita huko katika mkondo wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja wiki iliopita.   

 MKURUGENZI Mkuu wa Hospital ya Mnazi mmoja Jamala Adam Talib akitowa shukrani kwa Uongozi wa Zantel kwa msaada wao katika kipindi hichi kigumu cha janga la Msiba wa Wahanga wa Meli.

WAKUU wa kampuni ya Simu ya Zantel  wakiwa katika viwanja vya hospital ya mnazi mmoja kutoa msaada wa dawa. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.