Habari za Punde

HEROES WAISHINDIKIZA SWISS VETERANS 2-0

Na Mwajuma Juma

MAVETERANI wa timu ya Uswisi, wamemaliza ziara ya wiki mbili hapa Zanzibar, kwa kushindikizwa kwa kipigo cha mabao 2-0, mikononi mwa timu ya Taifa ya Zanzibar, ‘The Zanzibar Heroes’.

Pambano hilo lililochezwa katika uwanja wa Mao Dzedong juzi, ulikuwa burudani tosha machoni kwa mashabiki wachache waliohudhuria uwanjani hapo.


Zanzibar Heroes iliyokuwa chini ya kocha Hemed Suleiman 'Moroko', imo katika maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Chalenji yanayotarajiwa kuanza Novemba 26, jijini Dar es Salaam.

Zanzibar Heroes iliyjipatia bao moja kila kipindi, ambapo la kwanzai lilifungwa na Makame Hamad katika dakika ya 36, huku Mohammed Abdulrahman 'Mbambi', akiongeza la pili mnamo dakika ya 74.

Hicho kilikuwa kipigo cha pili kwa wakongwe hao, kati ya michezo mitatu waliyocheza, ambapo awali walishindwa na timu ya vijana (U-20) kwa mabao 2-1, kabla kupata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Wazee Sports ya Zanzibar.

Msafara wa timu hiyo uliokuja nchini kwa ziara ya kimichezo, kibiashara na kitalii, ulitarajiwa kuagwa jana usiku na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Abdilahi Jihad Hassan, katika hoteli ya Tembo iliyoko Mji Mkongwe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.