SERIKALI ya Zanzibar imeendelea kufichua kilichotokea katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi waliotaka kujiunga na Elimu ya juu kwa mwaka huu kwa kudai baadhi yao walishindwa kutimiza sifa walizotakiwa kuwa nazo huku wengine wakiwa na vyeti bandia.
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zahra Ali, aliyasema hayo jana wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Kiwani Hija Hassan Hija aliyetaka kujua kama serikali imepata msaada wowote kutoka mfuko wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania kwa vile suala hilo
ni la mambo ya Muungano.
Akijibu hoja hiyo, Naibu huyo alisema ni kweli kumekuwa na tatizo la baadhi ya wanafunzi waliomb mikopo kushindwa kupatiwa fedha, lakini bado kulikuwa na wengine walioshindwa kutimiza masharti ya kupatiwa mikopo hiyo.
Alisema baadhi ya wanafunzi hadi sasa wameshindwa kuwasilisha barua kutoka katika vyuo walivyodai kupata nafasi za kujiunga navyo, huku wakiwa tayari wameomba kupatiwa fedha.
Aidha, madudu mengine ambayo Naibu huyo alisema waliyagundua katika maombi ya wanafunzi hao baadhi yao waliwasilisha vyeti bandia jambo ambalo limesababisha kukosa fedha kwa ajili ya kujiunga na vyuo walivyoomba.
Naibu Waziri alisema, wamelazimika kuchukua tahadhari kutokana na hivi sasa shilingi bilioni 7/bn. ambazo bado hazijarejesha huku bajeti ya Wizara hiyo ikiwa imetenga shilingi bilioni 4/-
Alisema fedha kutoka katika mfuko wa Elimu ya juu zimekuwa hazichangii Ofisi za kikanda na Wizara hiyo imekuwa ikipata fedha hizo kutoka katika Wizara ya Fedha ya Zanzibar.
Kuhusu suala la ujenzi wa Chuo cha Teknolojia, Nelson Mandela kwanini kisijengwe Zanzibar , alisema hayo yaliofanyika yalikuwa ni maamuzi ya serikali ya Muungano kutumia eneo la sasa kilipo Chuo hicho.
Hata hivyo, alisema ujenzi wa Chuo hicho umetumia shilingi bilioni 67 na Zanzibar inatarajia kuwasomesha wanafunzi 26 kati ya wanafunzi 105 waliopatiwa nafasi ya kujiunga na Chuo hicho ambacho kinaanza kwa mwaka huu wa masomo.
Akiendelea kujibu suala la msingi la Mwakilishi huyo alietaka kujua Zanzibar inashiriki vipi katika ujenzi wa Chuo cha Sayansi ya Uhai kinachojengwa Arusha, ambapo Waziri huyo alisema Zanzibar haishirikishwi moja kwa moja kutokana na taasisi hiyo kuwa ni ya kikanda na inawakilishwa na serikali ya Muungano.
Alisema kutokana na chuo hicho kuwa ni kipya bado wanafunzi wengi wa Zanzibar hawajakitambua na wanachotaka kufanya hivi sasa ni kuangalia kuanzishwa utaratibu wa kukitangaza.
Wasipewe pesa, kwanza hawarejeshi mikopo.halafu wakirudi kusoma hawaleti mabadiliko yoyote!..kazi kuharibu pesa..tuu!
ReplyDeleteMtoa maoni apo juu, je! unajenga au unabobomoa?
ReplyDeleteLengo letu sote ni kujenga, lkn. tunatofautiana mitazamo juu ya ujenzi wenyewe. Mm nataka warejeshe mikopo ili na wenzao wapewe. Pili wanaopata mikopo na kusoma wakimaliza, wabadilike, na kuleta maendeleo ya kweli.Tusitoe mikopo ilimradi tuu!
ReplyDelete