Habari za Punde

MRADI WA JOZANI FOREST PARK KUWANUFAISHA WANANCHI

Yunus Sose

MRADI unaoshughulikia ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika eneo la hifadhi ya msitu wa Jozani (Jozani Forest Park), umewataka wananchi wa vijiji vya Pete, Muungoni na Kitogani kushirikiana kikamilifu na mradi huo ili kuendeleza uasili wake na kuepuka uharibifu.


Meneja wa mradi huyo Hassan Mussa Haji, alieleza hayo huko Pete, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo litakalofaidika na mradi huo.

Alisema mashirikiano baina ya mradi huyo na wananchi wa vijiji hivyo ndiyo yatakayosaidia kupiga vita uharibifu wa mazingira katika eneo hilo, hali ambayo ndiyo itakayoleta maendeleo ya taifa na wananchi hao.
Meneja huyo alisema mradi wa ‘Jozani Forest Park’ kupitia muwekezaji watahakikisha wanaendesha shughuli zao kwa lengo la kukukuza utalii wa hifadhi msitu asili mpango ambao kwa kiwango kikubwa utawanufaisha wananchi wa vijiji vya Pete, Muungoni na Kitogani.

“Bado wananchi hawajatufahamu vizuri malengo ya mradi huu, wamekuwa na wasiwasi hali inayowafanya wachanganye mambo, kwa kifupi mradi utawaendeleza vijana na wananchi wa vijiji hivyo”, alisema Meneja Hassan

Alisema mbali na mradi wa ‘Jozani Forest Park’ kushughulikia uhifadhi wa msitu asili, lakini wameshajipanga vuzuri katika kuwaendeleza vijana wa vijiji hivyo ikiwa ni pamoja na kuanzisha skuli maalum itakayokuwa inatoa elimu ya fani mbali mbali ikiwemo elimu ya kompyuta bila ya malipo.

Akizunguzia juu ya kuwepo kwa mradi huo Meneja Hassan alisema mradi wao unaendesha shughuli zake kisheria baada ya kufuata taratibu zote za usajili ambazo zinauhalilisha mradi huo kufanyakazi katika eneo hilo.
Alisema kwamba shughuli zao hizo zinazogusa shughuli za kitalii haziingiliana na miradi mingine ya kitalii inayoendeshwa katika maeneo ya vijiji hivyo kama inanvyodaiwa na baadhi ya wananchi wengine.

Hata hivyo Meneja huo alikiri kuwepo kwa misingi mibovu iliyojitokeza hapo awali kulikosababishwa na uongozi uliopita hali ambayo imekuwa ikileta migongano ya mawazo kwa baadhi ya wanavijiji.

Licha ya kuwepo mgongano huo wa kimawazo lakini wananchi wengi wa Pete wameunga mkono kuwepo kwa mradi huo na wamekuwa wakiwalalamikia baadhi ya watu wa maeneo hayo ambao wamekuwa wakisababisha hali hiyo kwa makusudi ya kuangalia maslahi yao binafsi kuliko maendeleo ya jamii ya watu waliowengi.

“Huu mradi siyo mbaya kwetu na umeonyesha matumaini mazuri lakini baadhi ya watu katika vijiji vyetu wamekuwa wakiwayumbisha waendeshaji wa mradi huo na kutia kasumba mbaya lakini hauna ubaya wowote kuwepo kwake pengine wao kwa kukosa maslahi yao binafsi ndiko kunawasababisha kufanya hivyo alisema kijana mmoja wa kijiji cha Pete”, alisema Meneja huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.