BAADHI ya Wabunge wa Zanzibar wamesema dhamira ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akichangia mswada wa sheria wa kuundwa kwa Tume ya kuratibu mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya, Mbunge wa Chaani, Ali Juma Chepe alisema CHADEMA ni chama chenye dhamira ya kuvunja Muungano.
Alisema haiwezekani maoni yaliyowasilishwa na kambi ya upinzani na Tundu Lissu kwa asilimia 75 kuonesha kuisakama Zanzibar na kueleza dhamira hiyo ya kuvunja Muungano lazima ipingwe na wananchi wa Zanzibar kwa kukikataa chama hicho.
Mbunge huyo alisema serikali ni vyema ikafikiria kumtaka msajili wa vyama ili aweze kukifanyia uchunguzi chama hicho kama kinasifa ya usajili kwani inawezekana kuwa hakuna mzanzibari anaekiunga mkono.
Mbunge huyo aliishangaa hotuba ya Lissu ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa ikitaka Zanzibar inyimwe haki kadhaa katika mchakato wa kupatikana katiba mpya ya Tanzania.
Chepe alisema kwa mujibu wa maoni ya kambi hiyo CHADEMA inaikataa Zanzibar na kitambue kuwa kipo njiani kufa kwani Wazanzibari hawatakuwa tayari kuona kinakipa nguvu ya kuweza kuwadhamini katika kusajili.
Mbunge huyo alisema inasikitisha kuona hivi sasa chama hicho kimekuwa kikiwatukana na kuwadharau wazanzibari bila ya kuthamini mchango iliyowapa wakati wakiomba kupatiwa usajili.
Alisema Zanzibar haiwezi kubakia na unafiki wa chama hicho na ni vyema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, kuangalia uwezekano wa kukirudishia chama hicho mchango wa shilingi milioni 5 zilizotolewa kwa ajili ya waathirika wa Mv. Spice Islander.
“Zanzibar wakati tuna maafa ya meli ya Mv. Spice Islander, tuliukataa msaada wa Vodacom baada ya kuendelea kuonyesha walimbwende ilionekana walidharau, Wazanzibari sasa na leo hii dharau hii inaendelea kutolewa na CHADEMA kwa mara ya tatu sasa tukatae msaada huu”, alisema Mbunge huyo.
Nae Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingston Joseph Selestine, alisema haiwezekani kuacha siasa za Tanzania kufanywa ni za kidalali kwa kutafuta mataifa ya nje kuziendesha kama inavyotaka kufanywa na chama hicho.
Alisema kinachojitokeza hivi sasa juu ya vurugu za CHADEMA ni baada ya kukosa ajenda ya kuiendeleza baada ya hapo awali kupokea agenda hiyo kama ni sehemu ya kuishinikiza serikali kukubali mabadiliko ya katiba kwa lazima.
Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa, alisema kama CHADEMA inataka serikali ya umoja wa kitaifa kama ilivyojitokeza Zanzibar ni vyema ikaeleza wazi.
Nae Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi, Zahra Ali Hamadi, alisema Lissu anapaswa kutambua Zanzibar ni nchi huru yenye Rais wake, Baraza la Mawaziri na Baraza la kutunga sheria na haiwezekani kuona kunakuwa na maneno ya dharau kwa serikali ya Zanzibar na watu wake.

ndio vizuri hivyo kwa upande wetu zanzibar pia...kwa vile hatujaridhika na Muungango huu fake....we mbunge vipi unasinzia nini ukiwa huko bungeni
ReplyDeletewe kwani hujui kama wazanzibar hawautaki muungano huu fake usiokuwa na faida yeyote ile kwetu.
Nyinyi wabunge wa ccm ni kwasababu hayo maneno yamesemwa na Chadema ndio munakuwa wakali?mbona hao hao ccm wenzenu wamesema nbovu dhidi ya zanzibar kuliko hayo na hamjasema kitu?au munataka masifa tu ,uzanzibar kwanza nduguzangu uccm uchadema ucuf hauna nafasi,kamamunauchungu kweli na zanzibar.
ReplyDeleteHawa wabunge wa CUF hawana mpango wowote wala hawapo katika kuitete zanzibr waongo tu wao wote wanatetea matumbo yao tu na kwasasa wanaonekana wazi wanajipendekeza kwa CCM , Hata nyinyi CUF karibuni hivi mtakosa wazamini Tanganyika.
ReplyDeletejamani ni lazima mujue kwa sasa wazanzibar wote ni wamoja,sasa huko bungeni CCM na CUF kueni kitu kimoja kuitetea zanzibar,jamani mtatuzamisha wazanzibar tuko hali ngumu,hebu jitahidini ili mujitoe katika mikucha ya wanyonyaji,na pia mukumbuke hakuna atakae ishi milele hapa duniani usiangalie maslahi yako tu,na jua utakwenda ulizwa juu ya uongozi uliopewa ni wazanzibar. Jamani tuweni kitu kimoja "UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU" ahsanteni
ReplyDeleteUzanzibari kwanza na mengine baadae. Tunachohitaji wazanzibari kwa sasa ni umoja utakaotukomboa. Hao chadema acheni wapige makelele lakini muhimu wazanzibari msikubali kurejeshwa mlikotoka.
ReplyDeleteMungu ibariki zanzibar
Amin