Habari za Punde

KATIBU WA KAMISHENI YA UTUMISHI WA UMMA AAPISHWA LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mtoro Almasi Ali,kuwa Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar

Na Rajab Mkasaba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Hafla ya kuapishwa kwa Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, Zanzibar ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.


Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedham Uchumi na Mipango ya Maendeleo Mhe. Omar Yussuf Mzee na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haji Omar Kheri.

Viongozi wengine waliohudhuria kuapishwa kwa Katibu huyo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib pamoja na viongozi wengine wa serikali.

Kabla ya Uteuzi huo Mtoro Almas aliwahi kuwa Meneja wa Mkuu wa Kiwanda cha Soda Zanzibar, Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Zanzibar, pia aliwahi kuwa Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar kilichopo Tunguu.

Uteuzi wa kiongozi huyo ulianza rasmi Novemba 20, Mwaka huu ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Shein alifanya uteuzi wa Katibu huyo wa Kamisheni ya Umma, Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 22 cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Zanzibar, No. 2 ya mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.