Sala ya Eid Al Hajj Kitaifa Itafanyika katika Viwanja vya Gombani ya Kale na kuhudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wananchi wa Kisiwani Pemba.
Baraza la Eid Al Hajj litafanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba Mkoa wa Kaskazini.
Mgeni rasmin katika baraza la Eid Al Hajj ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
Blog ya Jamii ya JIKUMBUKE inawatakia Waislam wote duniani kote Eid Njema, na inawapa Mkono wa Eid.
EID KARIM. EID MUBAARAK
No comments:
Post a Comment