Habari za Punde

SHAMRASHAMRA ZA KUTIMIZA MIAKA 20 YA JUMUIYA YA COWPZ KUTOWA MISAADA KWA WANAWAKE WA SOBA HOUSE MOMBASA

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuwaendeleza Wanawake Zanzibar.( COWPZ ) Balozi Amina Salum Ali, akimkabidhi Vyarahani Msaidizi Mlezi wa Nyumba ya Soba House ya Wanawake ya Mombasa, walioamua kuacha matumizi ya dawa za kulevya Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za Jumuiya hiyo kutimiza miaka 20 tangu kuyazishwa Zanzibar.      
Mlezi wa Nyumba za Soba House Zanzibar Bi Fatma Sukwa, akiwahamasisha Vijana wake wakati wa sherehe za kukabidhiwa Vyarahini kwa ajili ya kujifunza ushoni wanapotoka katika makaazi hayo. 
Msaidizi Mlezi wa Nyumba ya Soba House za Wanawake akitowa shukrani kwa msaada waliopewa na Jumuiya ya COWPZ.  
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya COWPZ Balozi Amina Salim Ali, akitowea nasaha zake kwa Vijana wanaoishi katika Nyumba za Sober House baada ya kuwakabidhi Vyarahani Wanawake ili kujikombowa na matumizi dawa za kulevya, ili kujushughulisha na kazi za Ushoni.
Mmoja wa Wanawake wanawaoka katika Nyumba za Sober House akitowa shukrani kwa niaba ya wezake kwa msaada waliopata wa Vyarahani kutoka kwa Wanawake wazao wa COWPZ. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.