Habari za Punde

AL JAZEERA YAKUMBWA NA TSUNAMI

Na Abdi Suleiman, Pemba

BAADA ya kuanza vyema mechi za kwanza za ligi ya soka daraja la kwanza taifa Pemba, timu ngeni ya Al Jazeera, imeshindwa kuizuia tsunami ya Madungu United, kwa kupigwa mabao 5-1.

Katika pambano hilo lililopigwa kwenye dimba la Gombani lenye mng’aro wa nyasi bandia, Madungu ilianza kuzichana nyavu mara mbili ndani ya dakika sita.

Mabao hayo yalifungwa na Said Khamis katika dakika za nane na 13, kabla Vuai Abdallah kuongeza la tatu dakika chache kabla mapumziko.


Kasi ya Madungu iliendelea tena katika ngwe ya lala salama, na kuandika bao la nne ambalo lilivurumishwa nyavuni na Kassim Juma katika dakika ya 57, na kufuatiwa na bao la kufutia machozi kwa Al
Jazeeta mnamo dakika ya 78.

Mchezaji Yakub wa Madungu alihitimisha karamu ya magoli kwa kuipachikia timu yake bao la tano katika dakika ya 84.

Na katika mchezo mwengine wa ligi hiyo, ikaichapa Mila magoli 4-2.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.