Na Asya Hassan
WALIMU wametakiwa kubuni mbinu mbadala za kufundisha ambazo zitawawezesha kuongeza uwelewa na ufahamu zaidi wanafunzi.
Katibu wa Baraza la wawakilishi Ibrahim Mzee Ibrahim alieleza hayo alipokuwa katika mahafali ya wanafunzi wa maandalizi wa skuli ya Glorious Academy yaliofanyika katika ukumbi wa Bwawani.
Alisema upoumuhimu kwa walimu kuchukuwa juhudi mbalimbali za kufundisha ili kuiendeleza sekta ya elimu na kuweza kuwajenga wanafunzi katika uelewa mzuri.
Alisema kuwa mwalimu ndie msingi wa mafanikio na ujuzi wowote katika maendeleo ambayo anayapa mwanadamu katika kuendeleza maisha yake.
''Kuna kila aina ya fani,viongozi,wakulima na hata madereva basi lazima upitie kwa mwalimu, mwalimu ndie kiongozi katika jamii,''alisema katibu.
Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi kuwa na mashirikiano na walimu ili kuendeleza malengo yaliokusudiwa.
Akisoma risala mwalimu wa skuli hiyo alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa chumba cha huduma ya kwanza pamoja na wauguzi.
Alisema kuwa ukosefu wa kiwanja kikubwa cha michezo na askali wa barabarani kwa ajili ya kuwavukisha njia watoto wanapoingia na kutoka skuli.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa skuli hiyo Omar Kingi alisema kuwa ifikapo january atafanya jitihada katika kutatuwa baadhi ya changamoto hizo kuzipatia ufumbuzi.
Skuli ya Glorious Academy imeanzishwa mwaka 2009 ikiwa na wanafunzi 480 wakiwemo maandalizi,elimu ya msingi na elumu ya sekondari hadi kufikia leo wanawafunzi 1445.
Assalam Alykum.
ReplyDeleteMbinu za kufundisha hapo nyumbani hizi kama tutataka kuzifuata,
Kwanza kabisa masomo yote yasomeshwe kwa lugha Kiswahili kama wenzetu wote ulaya na nchi nyingine wanavyofanya kuwasomesha watoto wao kwa lugha zao ili kuwapa nafasi ya kufahamu zaidi kile wanachofundishwa kutokana na kuwa lugha inawarahisishia kutambua mara moja,kama lugha nyingine.kiingereza,kiarabu,kigaransa au nyingineyo yoyote inahitajika kuwafundisha watoto wetu,basi lugha hizo zifundishwe kama ni lugha tu na sio kuzichanganya na masomo ya vijana wetu huko Africa,kama sisi tuliotembea sana hatujawahi kuona nchi inafundisha wanafunzi wao kwa lugha ya kifaransa na hali ni waingereza au waspain,mjerumani kamwe hatomfunza mwanafunzi wake kwa lugha ya kigeni ya kiarabu wa kidutch na ndio mifano hio kwa dunia nzima,wacheni kuwachanganyia vijana huko nyumbani science kwa kiengereza na masomo mengine wakati somo hilo hilo tutatoa madaktari wengi sana kama watasomeshwa kwa lugha yao ya taifa,aidha walimu wote waipende kazi yao na wajue majukumu yao,wasiende hapo shule kama wanalazimishwa hio kazi,washirikiane vizuri na waonyeshe upendo kwa wanafunzi wote,waonyeshe uso wa bashasha wanapofundisha watoto na sio kuingia darasani huku ukiwa umekunja uso kama unakula limao,hata wewe mtoto wako kama atafanyiwa hivyo na mwalimu mwingine hutofurahia,walimu wawe wanacheka na wanafunzi ili watoto wawe na hamu ya kila siku kukutana na walimu wao kutoka na urafiki watakaoujenga hapo shuleni,na sio mwanafunzi kuchukia anapoingia mwalimu darasani kwavile anakuwa anawanyanyasa vijana hao,wakati wa heshima mwalimu ni lazima apewe heshima kubwa kama sheria za shule zitakavyosema na wakati wa masomo na mwalimu asiwe na sababu ya kukasirika kiholela wakati hakuna wanafunzi wowote waliovunja sheria za shule.aidha masomo ya lugha za kigeni kuwa na walimu waliobobea na wenye vipaji vikubwa vya kuwafundisha watoto wetu tokea madarasa ya kwanza ili kujijengea misingi mizuri ya somo hilo mbele ktk madarasa mengine ya juu zaidi.isitoshe wazazi wawe na jukumu la kuwauliza watoto zao walichokisoma kila siku ili kuwatilia mkazo vijana hao kuweza kufahamu zaidi na kujijengea misingi bora ya kuja kuliongoza taifa letu hapo baada,kwani hao vijana wa leo ndio viongozi wetu wa taifa la kesho,ndio viongozi wa watoto wetu na watoto wa watoto/wajukuu zetu wapenzi.
Ahsante.
Mm. niwapongeze wamiliki wa Glirous academy, kwa uwamuzi wao wa kuanzisha skuli hii. ni miongoni mwa waznz. wachache walioamua kuwekeza ktk. elimu badala ya kufungua maduka na kuoa-oa bila mpangilio. Hii sasa ni changamoto kwa waznz wenye uwezo kupeka watoto wao huko na kuipunguzia serikali mzigo wa kusomesha.
ReplyDeletePili, ni kwa ndugu zangu walimu, tubadilike na kuwa serious ktk kufundisha. Tuwacheni mazoea tutumie mbinu mpya na kutumia mitandao ya internet ie. 'Google' kutafuta materials. Ni kweli kipato ni kidogo lkn. tumeona serikl. ilivyojitahidi kwa uwezo waku..haijawahi tokea!
Mm naaminiani mw. unapokua 'competent' hata soko la ajira kwako linakua.