Na Mwajuma Juma
CHAMA cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA), kimeandaa mashindano ya mchezo huo kwa ajili ya kusherehekea Mapinduzi ya Zanzibar.
Mashindano hayo ambayo yatafanyika mwanzo mwa mwezi wa Januari yatashirikisha timu za Taifa za nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Kaimu Katibu Mkuu wa CHANEZA, Rahima Bakari, alisema, mashindano hayo ambayo ni ya kwanza kufanyika wakati sherehe za Mapinduzi, yatashirikisha wachezaji wa kike na kiume wa timu za taifa.
Alizitaja timu hizo kuwa ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Zimbabwe na timu ya taifa ya Zanzibar ambayo itawashirikisha wanaume.
“Ni mara yetu ya kwanza kufanya mashindano haya ambayo tumepata baraka kutoka kwa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo”, alisema.
Alisema kuwa pamoja na kuwa wameandaa wao CHANEZA, lakini masuala yote ya zawadi pamoja na mambo mengine yatasimamiwa na kamati ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wake Mohammed Raza.
No comments:
Post a Comment