Habari za Punde

COSSOVO YAOTA DARAJA LA PILI TAIFA

Na Haji Nassor Pemba

TIMU ya soka ya Cossovo ya Chumbageni Wambaa, ambayo inashiriki ligi daraja pili wilaya ya Mkoni, kisiwani Pemba, imesema, kwasasa wanachojadili ni ushindi kwenda mbele hadi kufikia ligi daraja la pili taifa Pemba msimu ujao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mmoja kati ya viongozi wa timu hiyo, Mohamed Abass, alisema, tokea kuanza kwa msimu huu wa ligi wamekuwa wakifanya vizuri na hivyo kujenga matumaini ya kufikia hatua hiyo.

Alisema, pamoja na ugeni wao kwenye ligi hiyo, lakini kutokana na maandalizi makubwa walioyafanya miezi miwili kabla, yameanza kuzaa matunda na kuwapa uhakika wa kupanda daraja msimu ujao.

Cossovo ilianza ligi hiyo kwa kuipa kichapo cha magoli 3-2 timu kongwe ya Makombeni ya Pindua kabla ya kuimiminia mvua ya magoli timu ya Charanga nayo ya Makombeni kwa magoli 6-1 na baadaye kwenda sare ya 0-0 na Jiondeni, katika mchezo uliopigwa uwanja wa Makombeni.

Cossovo ambayo ilipanda daraja msimu uliopita ikitokea daraja la tatu, hadi sasa inaongoza ligi daraja la pili wilaya ya Mkoani kanda ya Makombeni ikiwa na pointi saba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.