Habari za Punde

MAPAMBANO DHIDI YA MABADILIKO YA TABIA NCHI YANAHITAJI MASHIRIKIANO

Hassan Hamad (OMKR).

Mtaalamu wa mazingira kutoka nchini Uingereza Bwana Paul Watkiss ameelezea umuhimu wa kuwepo mashirikiano ya karibu baina ya serikali, taasisi binafsi na wananchi katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema iwapo wadau hao watafanya kazi pamoja, athari za mabadiliko ya tabia nchi zinaweza kupungua Zanzibar kwa vile mabadiliko hayo hutokana na shughuli za kila siku za wanadamu.


Bwana Paul ambaye anatafanya utafiti kuhusu mabadiliko ya tabia nchi hapa Zanzibar ameeleza hayo alipokuwa na mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji huko ofisini kwa Migombani.

Amesema miongoni mwa changamoto kubwa za kimazingira kwa Zanzibar ni pamoja na ukataji miti ovyo hasa katika maeneo yaliyo kando ya bahari pamoja mmomonyoko wa ardhi katika maeneo hayo.

Kwa upande wake Mhe. Fatma Ferej amesema ripoti za tafiri hizo ni muhimu katika kuweka sawa mipango ya serikali na mipango yake ya maendeleo, na kuahidi kutoa ushirikiano kwa mtafiti huyo ili aweze kufanya utafiti huo kwa ufanisi.

Wakati huo huo Bw. Paul amewasilisha mpango wa utafiti wake kwa kamati ya mabadiliko ya tabia nchi inayowashirikisha makatibu wakuu na watendaji wa idara ya mazingira.

Akiwasilisha mpango huo amesema mabadiliko ya tabia nchi yana athari kubwa katika maendeleo ya kiuchumi, ikizingatiwa kuwa sekta ya kilimo ambayo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi huathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.