Habari za Punde

MAALIM SEIF ASEMA VYAMA VINGI SI UGOMVI

Anaetaka vurugu atafute nchi ya kuishi

Hasssan Hamad, OMKR

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema mfumo wa vyama vingi haukuja kwa lengo la kuwagombanisha wananchi bali kushindanisha sera ambazo zinalenga kuwaletea wananchi maendeleo.

Alisema vyama vyote vya siasa vina lengo moja la kuleta maendeleo kwa wananchi na hivyo hakuna sababu kwa wananchi kugombana kutokana na itikadi za vyama, isipokuwa kupima sera za vyama ili kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua chama chenye mwelekeo wa kujali maslahi ya wananchi.


Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha CUF alitoa changamoto hiyo katika kijiji cha Njinjo kilichoko kaskazini mwa wilaya ya Kilwa, alipowahutubia wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara uliowajumuisha viongozi wa Mkoa wa Lindi na vyama vya CCM na CUF.

Alisema wilaya ya Kilwa yenye majimbo mawili ya uchaguzi moja likiwa chini ya CCM na jengine CUF, inaweza kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa upande wa Tanzania Bara kutokana na mashirikiano mazuri yanayooneshwa na viongozi wa kisiasa katika Wilaya hiyo.

“Siasa si ugomvi bali ni maendeleo,” alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa wakati siasa za malumbano sasa umekwisha na yeyote mwenye lengo la kuleta vurugu atafute nchi nyengine aende kwani Tanzania inajivunia
amani iliyopo, ambayo imekuwa mfano kwa nchi za Afrika.

Alifahamisha kuwa upo uwezekano wa kupingana bila kupigana ikiwa vyama vya siasa vitaweka mbele maslahi ya taifa na kuondokana na tamaa binafsi zisizojali maslahi ya raia.

“Wapo wenzetu wanasema eti CUF ni CCM ‘B’ kwa kuwa kule Zanzibar tumeshirikiana kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wao walitaka siku zote wazanzibari tuendelee kuuwana? alihoji.

 Akizungumzia kuhusu maendeleo ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif alisema katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Zanzibar inatarajiwa kuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi na
kuwawezesha zaidi ya nusu ya vijana wa Zanzibar kupata ajira katika serikali na taasisi binafsi.

Alisema ndani ya kipindi hicho Serikali inatarajia kukamilisha ujenzi wa barabara zote za vijijini sambamba na kuliondoa kabisa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote ya Zanzibar.

Kabla ya mkutano huo Maalim Seif aliweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji cha Kipindimbi Wilaya Kilwa na kuahidi kuchangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia umalizaji wa jengo hilo ambalo tayari limeshaezekwa.

Alisema wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu kufuata huduma za afya zaidi ya kilomita kumi hali ambayo imekuwa ikisababisha vifo hasa kwa akina mama na watoto, na kutaka jengo hilo
limalizwe haraka ili liweze kutoa huduma.

Viongozi mbali mbali waliahidi kuchangia ujenzi wa jengo hilo akiwemo Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM) Mumtadha Mangungu ambaye aliahidi kuchangia tani tatu za saruji ambapo Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF),
Suleiman Bungala (Bwege) aliahidi kuchangia tani mbili za saruji, huku halmashauri ya Wilaya hiyo ikiahidi kukamilisha kabisa jengo hilo na kulikabidhi kwa wananchi mwaka

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.