Habari za Punde

TUNALIPA ADA KWA DOLA ZANZIBAR UNIVERSITY

CHUO Kikuu cha Zanzibar ni chuo kilichoanzishwa mwaka 1998 na taasisi ya dini ya Kiislamu iitwayo Darul Iman.

Pamoja na kuwa chuo hiki kimeanzishwa zaidi ya miaka kumi iliyopita Wanafunzi wa chuo hiki tumekuwa tukikumbana na changamoto mbalimbali kutoka katika uongozi wa chuo na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB).

Tukianza na matatizo yanayosababishwa na chuo, tunakumbwa na tatizo la kulipa ada na michango mingine ya chuo kwa dola na hii ni kwa muda mrefu.


Malipo hayo yamekuwa yakituhusu wanafunzi Watanzania na wanafunzi wasio Watanzania,Utaratibu huu wa kulipa michango mbalimbali na ada ya chuo kwa dola, umekuwa ukitupa tabu sana sisi wanafunzi wa Kitanzania.

Hii ni kwa sababu thamani ya shilingi imekuwa ikishuka sana ukilinganisha na dola, hivyo wanafunzi tunashindwa kumudu gharama za maisha ya chuo kwani inatulazimu kubadili shilingi ya Kitanzania kwenye dola.

Katika suala hili tunaiomba Serikali ipige marufuku matumizi ya dola kwenye chuo hiki kwa wanafunzi Watanzania ili iwepo ada kamili inayojulikana kwa fedha za Kitanzania.

Tatizo la pili ni ucheleweshwaji wa makusudi wa pesa kwa wanafunzi wanaopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo (HESLB). Bodi ya mikopo imeanzisha utaratibu mpya wa kuajiri mwakilishi wake katika kila chuo, ili kushughulikia masuala ya bodi, lakini hapa chuoni hayupo kwani tumekuwa tukihangaika na hatumuoni

Pamoja na kwamba chuo chetu kipo pembezoni mwa nchi na kuonekana kimejitenga kama kisiwa, tunaiomba Serikali yetu sikivu itusaidie kabla hatujaamua kufanya migomo na maandamano ambayo siyo jadi yetu.

CHANZO: Mwananchi

5 comments:

  1. Naamini serikali italiangalia suala hili. Ni kweli Migomo na maandamano siyo jadi yetu lakini pia hatuwezi kuruhusu kitu cha namna hiyo kwa vile kinaweza kuleta madhara makubwa zaidi.

    ReplyDelete
  2. How come mtanzania ndani ya Tanzania atakiwe atumie pesa ya kigeni wakati Tanzania kama nchi yenye pesa yake halali inayojulikana kama SHILINGI. Hii sasa ni kujidhalilisha na kujidharau, kisha tunazungumza uchumi wetu upande, how wakati pesa yatu tunaiyoa thamani. Serikali jiangalieni yasije yakawa kama ya Zimbabwe.

    ReplyDelete
  3. Hili tatizo lina pande mbili. Upande wa walipaji na wenye chuo. Ukiangalia suala hili kwa macho ya wanachuo basi utaona kweli si haki kuwalipisha kwa dola kwasababu inabidi watu wanunue dola kila mara na huku ukizingatia kuwa bei ya dola inapanda kila siku kwahiyo mtu utakuwa hujui kabla uwe na kiasi gani cha fedha ambacho kitaweza kutosha.
    Lakini ukiangalia suala hili kwa upande wa wenye chuo pia kuna ugumu wake. Kwasababu kwa kuwa ni chuo cha kigeni basi inabidi matumizi yawekwe kwenye dola. Sasa wakiweka matumizi kwa shilingi itakuwa chuo hakiko stable kifedha kwasababu bei ya shilingi inaendelea kushuka.
    Sasa tusilaumu tu tuangalie mantiki pande zote. Kile ni chuo binafsi na sio cha serikali

    ReplyDelete
  4. Nimesikia ya kuwa chuo hicho wanasoma watanzania na wageni. Kwa wageni kwao isiwe na pingamizi kulipia dola, lakini kwa watanzania lazima wawe na bei maalumu kwa pesa ya kitanzania. Niliwahi kufanya kazi katika hotli moja kubwa ya kitalii Zanzibar, sheria ilikuwa wageni wote wanaotoka nje ya Tanzania malipo yao yanalipwa kwa dola, na wataznaia wote malipo yao yanakuwa kwa Tanzania shillings. Kwa hiyo sioni kwa nini chuoni hapo hilo lisiwezekane. Serikali wao ndio wawe mbele kutetea shilingi yetu pamoja na wananchi wake.

    ReplyDelete
  5. Mr Roy unachanganya vitu viwili tofauti. Kinachozungumziwa hapa sio malipo ya mshahara kwa wafanyakazi 10 au hata 50. Hapa inazungumziwa ada ya wanafunzi wasiopungua elfu. That is alot of money! Hebu fikiria hiyo hoteli uliyokuwa ukifanya kazi kama wageni wote (japokuwa ni idadi ndogo) wangeruhisiwa walipe kwa pesa za Tanzania, ingekuwaje? Na fikiria hili ukilinganisha na rate ya dola ilivyokuwa enzi hizo ulipokuwepo wewe. Wenye mahoteli wanaweza kumaintain business zao kwasababu wanalipisha kwa dola hasa kwa wageni wao wanaotoka nje(ambao ndio wengi)

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.