Habari za Punde

ZANZIBAR CENTRAL COMBINE YAZIFUAA SIMBA, YANGA

Na Salum Vuai, Maelezo

TIMU mchanganyiko ya daraja la Central Zanzibar kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 17, inatarajiwa kwenda Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kucheza mechi kadhaa za kirafiki.

Katibu wa Kamati ya Central Taifa Abdullah Thabit ‘Dula Sunday’, amesema timu hiyo inayojumuisha wachezaji 20, itakapokuwa huko, itapambana na timu ya vijana ya mabingwa wa soka Tanzania, Yanga.


Timu nyengine zitakazopimana ubavu na vijana hao, ni Simba, Azam FC pamoja na Rangers, ambapo michezo yote hiyo imepangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Uhuru.

Mechi kati ya Zanzibar na Simba, ndiyo itakayokuwa ya kwanza katika ziara hiyo, ambayo inatarajiwa kuchezwa kesho.

Thabit amewataja wanandinga waliomo katika kikosi hicho, ni Raphael Thomas, Abdallah Suleiman, Ibrahim Hilika, Suleiman ‘Rooney’, Khelef Naim, Abdulrahman Othman, Salum Bashoot, Muhene Majid, Mzee Kheir na Ibrahim Sangula.

Wengine ni Abdallah Kheir, Masoud Mohammed, Hafidh Suleiman, Jafar Ayuba, Omar Said ‘Zungu’, Juma Amour, Ali Salim, Othman Abdulrahma, Mohammed Juma ‘Kidishi’ pamoja na Costinho Mohammed.

Viongozi watakaoambatana na timu hiyo, ni Abdallah Thabit, Simai Vuai, Ramadhan Madundo, Abdi Shagaa na Odero.

Katibu huyo amesema, ni matumaini yao kuwa ziara hiyo itaisadia timu yake kujijenga vyema, huku akisema wanatarajia kushinda na kulinga’risha jina la Zanzibar kisoka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.