Na Othman Khamis Ame
Kikao cha Kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kimekutana chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohd Gharib Bilal.
Kikao hicho kilichohusisha Mawaziri, Makatibu Wakuu, Watendaji wa Serikali wakiwemo pia Wataalamu kilifanyika kwenye ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza Mjini Dar es salaam.
Wajumbe wa Kikao hicho walikubaliana kuthibitisha kumbu kumbu za Kikao cha Kamati ya pamoja ya SMT na SMZ cha Tarehe 2 Juni mwaka 2010 kilichokutana Bwawani Mjini Zanzibar.
Halkadhalika Wajumbe hao walipitia Taarifa ya Utekelezaji wa yatokanayo na Kikao hicho ambayo ni Ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia, Uvuvi katika ukanda wa Bahari Kuu na Ushirikiano wa Zanzibar na Taasisi za Nje.
Taarifa nyengine ni ajira kwa Watumishi wa Zanzibar katika Taasisi za Muungano, mgawanyo wa Mapato yatokanayo na faida ya Benki Kuu, Malalamiko ya Wafanyabiashara kutozwa kodi mara mbili walingizapo bidhaa zao Tanzania Bara, usajili wa vyombo vya moto, likiwemo pia ongezeko la gharama za umeme kutoka Tanesco kwenda ZECO na Uharamiawa na utekaji nyra meli.
Katika Majadiliano hayo Mwenyekiti wa Kikao hicho Dr. Mohd Gharib Bilal aliagiza mamlaka zinazohusika kutoa maelekezo ndani ya kipindi cha miezi mine kuhusu suala la utafutaji na uchimbaji wa mafuta na Gesi asilia.
Mapema Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar Mh. Othman Masoud Othman alisema taratibu zote na Baraka kuhusu suala hilo zimeshachukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Baraza la Mapinduzi na Baraza la Wawakilishi na kuliwasilisha Serikali ya Muungano kwa hatua za kisheria.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi alisisitiza haja ya kuwa na ratiba maalum ya vikao pamoja na kupunguza urasimu wa utekelezaji wa maamuzi yanayofikiwa katika vikao hivyo vya pamoja.
Balozi Seif alisema hatua hiyo itapunguza kero zilizopo na hatimae kuamsha ari ya kuimarisha Muungano kwa pande zote mbili.
“ Nirahisishieni kazi ndani ya Baraza la Wawakilishi kwa wajumbe wake wako Solidarity na hakuna Mjumbe wa CCM wala CUF katika suala lolote linalohusu Muuungano ”. Alisisitiza Balozi Seif.
Katika kikao hicho upande wa Wajumbe wa Serikali ya Muungano uliongozwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda wakati ule wa Zanzibar Uliongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
wazushi tu
ReplyDeletehawa wote ni wa kuripuliwa ,wauwawe tuu,majambazi wa nafsi zao,
ReplyDeletehili suali la mafuta si lishaamuliwa ndani ya baraza la wawakilishi? kuwa litolewe ktk mamabo ya muungano?? sasa huu mzunguko unatoka wapi mh Iddi??
ReplyDeletewazanzibar kuweni na akili hao wezenu wanataka faida kwao ya nn kikao hicho na suala la mafuta tayari limeshazungumza kuwa si la muungano,mheshimiwa IDD kuwa makin usijetuzamisha kwa kupewa fupa dogo na kuahidiwa uraisi kwa miaka ijayo kwan huna uhakika kuwa utafika,watetee wazanzibar wenzako ili upate hadhi ya zanzibar
ReplyDeleteSisi watu wa visiwani, hii tunaita geresha bwege. Wacheni kutubabaisha hamuna hata moja mufanyalo, munawaogopa watanganyika kama mwalimu wa chuoni.
ReplyDeleteMimi, kwanza naomba idadi, majina na CV za wataalamu wa Z'ar walioshiriki ktk kikao hicho, tuone kama watakua na msaada wowote.
ReplyDeletePili, nawaomba ndugu zangu waz'bari tufuatilie mambo ili angalau tukitoa michango yetu iweze kutoa njibu(solution) nini kifanyike.
Inasikitisha kuona kila mtu:"hatutaki" "twaonewa" tugawane mbao" na wengine wanaishia kutukana tu! sasa kwa mtaji huu, hata hao walioshiriki hicho kikao wakisoma haya maoni wataona kua hatupo 'serious'
Huu ni uzushi sema zanzibar na sie tunapenda kulalamika sana bila vitendo sie tunakuwa hatuna tofauti na wabaguzi wabara kuwepo zanzibar na kufanya kazi wengi hawapendi ila sie wazanzibari tupo wengi bara na yetu tunashukuru yanaenda tuwe waislamu jamani na kufikiria chuki zetu ipo siku itatuharibia kama waislamu, haki ni vizuri kuisimamia, Adhubany umesema kweli.
ReplyDelete