Othman Khamis Ame.
Vijana wanaomaliza masomo yao ya Elimu ya juu katika vyuo mbali mbali wametakiwa kutokuwa na hofu wakati watakapopambana na changa moto zitakazowakabili za ajira katika maisha yao mapya baada ya kumaliza masomo.
Wito huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif li Iddi katika mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu ch Elimu kiliopo Chukwani Wilaya ya Magharibi.
Mahafali hayo yamejumuisha Wahitimu 219 wa ngazi ya Shahada katika fani za Sayansi, Kiarabu na Jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ni vyema kwa Vijana hao kutumia busara na maarifa katika kukabiliana na chana moto hizo kwa lengo la kupata ufanisi.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Serikali inaendelea na juhudi mbali mbali za kubuni mbinu za ajira ili kupunguza wimbi la Vijana wasiokuwa na kazi.
“ Nataka muondoke hapamkielewa mapema kwamba mnaenda kupambana na changamoto ambazo tayari zimeshakuwepo kabla yenu nyinyi ”. Balozi Seif aliwaasa wahitim hao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliezeza matumaini yake kwa kundi hilo la Wataalamu wa fani tofauti ikiwemo ile ya Dini ambalo lina uwezo wa Kusaiia Jamii katika kufuata Maadili mema.
Alisema Jamii hivi sasa imekumbwa na mmong’onyoko wa Maadili hasa kwa kundi kubwa la Vijana ambao hujiingiza katika wimbi la Dawa za kulevya .
Balozi Seif alisisitiza kwamba wengi wa Vijana katika Kundi hilo hutumbukia katika Dawa za Kulevya na hatimae baadhi yao kuambukizwa Virusi vya Ukimwi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alilipongeza Shirika la Misaada ya Kiislam la Africa Muslim Agency’s kwa kusaidia masomo ya Elimu ya Juu hapa nchini kwa karibu miaka saba iliyopita na kupelekea kuzalisha wahitimu wapatao 1197.
Katika maoni yao Wahitimu hao kupitia fani ya utenzi ulioghaniwa na Muhitimu Mohd Ngarima waliiomba Serikali kuangalia vyema suala la mikopo ambalo limekuwa tatizo linalowakosesha utulivu kaika kujipatia Taaluma ya juu.
Pia walishauri kuimarishwa kwa mfumo wa upatikanaji wa huduma za maji safi suala ambalo limekuwa kikwazo chuoni hapo.
Mapema Mkuu wa Chuo Kikuu ch Elimu Chukwani Dr. Lezzedin Abdullrahman Maghazzudh alisema Uongozi wa Chuo hicho umelenga kuongeza kiwango na ubora wa Taalum katika Mihula ijayo
DrLezzedin alifahamisha kwamba sambamba na hilo Chuo kinakusudia kufungua milango zaidi kwa Vijana kujiunga na Chuo kwenye masomo ya lugha za Kiingereza na Kiarabu katika ngazi ya Diploma na Cheti.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza Watumishi Wataalamu ndani ya jamii.
Akitoa Salamu zake katika Mahafali hayo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Afrika {IUA} Profesa Mahd Satti Saleh alisema Taasisi yake iko katika Mipango ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kimataifa Zanzibar
{ Zanzibar International University }.
Profesa Satti alisema mipango hiyo inatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2015 kupitia Kamisheni ya Elimu Tanzania.
Miongoni mwa Wahitimu hao 219 Chuo Kikuu Cha Elimu Chukwani katika ngazi ya Shahada 83 ni wa fani ya Kiarabu, 30 fani ya Sayansi na 106 wa fani ya Jamii.
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
29/1/2012.
No comments:
Post a Comment