Habari za Punde

Kusini Hoi kwa Magharibi

Na Hadia Khamis

TIMU ya kombaini ya Wilaya ya Magharibi, imeichapa Wilaya ya Kusini mabao 2-1, katika mchezo wa kugombea Kombe la Mapinduzi la Abeid Amani Karume kwenye uwanja wa Mao Dzedong juzi.

Hata hivyo, Kusini ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufunga, katika dakika ya 15 kupitia kwa mshambuliaji wake Simai Abdallah, kabla Nassor Jamal kuisawazishia Magharibi mnamo dakika ya 25.

Bao lililoitoa Magharibi kifua mbele lilipachikwa kimiani na Ibrahim Hamad katika dakika ya 38 ya mchezo.

Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo katika uwanja wa Mahonda ambapo Wilaya ya Kaskazini B itaikaribisha Wilaya ya Mjini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.