Habari za Punde

Wafugaji Wadogo Wadogo Kutononeshwa

Na Haroub Hussein

WAZIRI wa Mifungo na Uvuvi, Said Ali Mbarouk amesema serikali imeweka mikakati endelevu ya kuhakikisha inawanyanyua wafugaji wadogo wadogo kwa kutoa misaada ya gharama nafuu itakayosaidia kuongeza nguvu katika ukuaji wa sekta hiyo nchini.

Aliyasema katika kufanikisha hatua hizo, serikali inashirikiana na wahisani mbalimbali ili kuwaelimisha wafugaji kutumia mbinu za kisasa ikiwa pamoja na upatikanaji wa vyakula vyenye gharama nafuu.


Aliyasema hayo kwenye makabidhiano ya mifuko ya chakula cha kuku zaidi 421 itakayogaiwa kwa wafugaji wa unguja, ambayo ilitotolewa na kampuni ya ‘Best Importants’ kutoka Marekani.

Alisema kuwa msaada huo utasaidia kuinua uzalishaji wa kuku wenye kiwango cha kimataifa na pia kuengeza soko la bidhaa hiyo nchini.

Hata hivyo, ameishukuru kampuni hiyo kwa juhudi zake za kuiunga mkono serikali kwenye harakati za kuimarisha maendeleo ya wazalishaji wadogo wadogo.

Kwa upande wake Meneja wa kampuni hiyo, David Elua alisema msaada huo umetolewa ikiwa ni majaribio katika mradi wa kuinua uzalishaji wa kuku wa kisasa Zanzibar wenye kiwango cha kimataifa ili kuweza kusaidia kuinua soko nchini.

Hata hivyo, ameahidi kuwapeleka nchini Marekani baadhi ya wafugaji kwa ajili ya mafunzo ya utengenezaji wa chakula cha kuku ili jumuiya hiyo iweze kujitegemea vwenyewe.

Nae Mwenyekiti wa jumuiya ya Wafugaji wadogo wadogo Zanzibar, Yussuf Amour ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwapatia huduma ya chakula kwa ajili ya mifungo yao.

Chakula hicho kinatarajiwa kugaiwa kila wilaya ikiwemo ya Mjini Magharibi, Kusini, Kati na Kaskazini zote ni kutoka Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.