Habari za Punde

Mfuko wa Karafuu Ndiyo Mkombozi kwa Mkulima.

Na Khatib Suleiman

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo katika hatua za mwisho kutayarisha mswada wa kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya Karafauu ambao utakuwa ndiyo mkombozi kwa wakulima wa zao hilo.

Akizungumza na gazeti hili,Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui alisema utafiti umefanywa na kuonesha kwamba kazi za mfuko hizo zitakuwa ndiyo suluhisho la wakulima wa Karafuu kupiga hatua kubwa ya maendeleo.


'Tumefanya utafiti wa kutisha na kubaini kwamba mfuko wa Karafuu ni muhumu sana kwa maendeleo ya kilimo cha zao hilo ikiwemo kuwanufaisha wakulima wa Karafuu na kuachana na tatizo la omba omba'alisema Mazrui.

Kwa mfano alisema hivi sasa wakulima hawawezi kukopeshwa na taasisi za fedha ikiwemo mabenki kutokana na kutokuwa na mtaji wa fedha za uhakika.

Lakini watakapokuwa na mfuko wa maendeleo wa Karafuu utakuwa ukiratibu shunguli hizo ambao utakuwa ukitoa mikopo kwa wakulima wa Karafuu bila ya matatizo.

'Mfuko huu utakuwa ukiratibu shunguli za kutoa mikopo kwa wakulima wa Karafuu baada ya kujisajili....utasaidia wakulima kujitayarisha kuweka kambi kuchuma Karafuu kwa kuajiri vibarua'alisema Mazrui.

Alisema mswada huo kwa sasa upo kwa wadau wakiwemo wakulima wa zao la Karafuu kwa ajili ya kutoa maoni yao kabla ya kwenda katika vyombo vya juu ikiwemo ngazi za Makatibu Wakuu.

Wakulima wa Karafuu katika kisiwa cha Pemba katika kipindi cha msimu wa mavuno ya Karafuu tayari wametia kibindoni zaidi ya sh.Bilioni 62 zinazotokana na mavuno ya Karafuu.

Wakulima hao wameingiza fedha hizo baada ya kuuza karafuu zao katika shirika la taifa la biashara (ZSTC) tani 4213,768 na kupata zaidi ya sh.62,971,983,250.00

1 comment:

  1. Suluhisho si uanzishawaji wa mfuko bali ni kuwapa wnanchi elimu juu ya namna bora ya kutumia fedha wanazo zipata.

    Muheshimiwa akumbuke, wakati wa ukoloni ulikua na mifuko ya namna hiyo, lkn. matokeo yake ilikuwa ni wananchi kushindwa kulipa madeni na hatimae kufilisiwa mashamba yao na wahindi na kama si mapinduzi basi wasingeyapata tena.

    Ukienda Pemba leo hii huwezi kuamini kuwa kisiwa kile ndicho kilichoifanaya Z'bar iongoze duniani kwa uzalishaji wa zao la karafuu. kwa kweli hali ni mbaya na unaweza kujiuliza wananchi walitumiaje kipato kilichotokana na zao la karafuu?

    Hasa ukizingatia ukweli kua kwa wakati huo serikali ilikua ikigharamia takriban kila kitu, ikiwa ni pamoja na matibabu na elimu, watu walishindwa hata kujenga nyumba zao wenyewe badala yake wakaamua kuwekeza 'KATIKA KUOWA TUU'

    Wapeni elimu watu acheni kabisa kuota ndoto za alinacha!..tutumieni historia kujifunza!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.