Habari za Punde

Msekwa Awakumbusha Wanachama Maadili

Na Khatib Suleiman

Makamo Mwenyeketi wa chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Pius Msekwa amewakumbusha wanachama wa chama cha Mapinduzi kuzingatia maadili ambayo ndiyo muongozo wa kuimarisha chama hicho.

Msekwa alisema hayo huko UZINI wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi kwa mgombeya wake Mohamed Raza,na kusema maadili katika chama yameshuka sana.


'Napenda kuwakumbusha wanachama wa chama cha Mapinduzi suala zima la maadili.....zipo ahadi tatu za mwanachama wa chama cha Mapinduzi ikiwemo kuzingatia maadili ya chama'alisema Msekwa.

Alisema chama cha Mapinduzi hivi karibuni kinatazamiwa kutoa muongozo utakaozingatia suala zima la maadili ya chama kwa wanachama pamoja na viongozi.

Mapema akizinduwa kampeni hizo Makamo Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Zanzibar Amani Abeid Karume alisema CCM ndiyo chama kinachotekeleza ahadi zake kwa wapiga kura.

Alitoa mfano katika mwaka 2005 wakati alipokwenda jimo la Uzini kuomba kura kwa wananchi katika uchaguzi wa rais,aliahidi kujenga barabara kwa kiwango cha lami pamoja na shule ya sekondari ya kisasa ,ahadi ambayo imetekelezwa kwa vitendo.

'Hiyo ndiyo CCM ambapo wakati inapoahidi jambo kwa wapiga kura basi hutekeleza kwa vitendo bila ya matatizo'alisema.

Aliwaomba wanachama wa chama cha Mapinduzi pamoja na wananchi kwa ujumla kumchaguwa Raza kwa sababu ndiyo chaguo la wapiga kura baada ya kupata ushindi mkubwa katika kura za maoni.

Akijitambulisha kwa wananchi pamoja na kuomba kura,Raza aliahidi kushirikiana na wananchi wa jimbo la UZINI kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.

'Nimeomba kazi ya Uwakilishi kwa ajili ya kuwaleteeni maendeleo katika sekta mbali mbali....mkinichaguwa kamwe sitawaangusha na nitatimiza matakwa yenu'alisema Raza.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.