Habari za Punde

Uzinduzi wa Kampeni ya CCM Jimbo la Uzini Wilaya ya Kati Unguja.

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Uzini na kufungwa kiskafu na Vijana wa Chipukizi. 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Amani Baeid Karume, akizungumza na Mgombea wa CCM Jimbo la Uzini Mohammed Raza, alipowasili katika viwanja vya Uzinduzi wa Kampeni Skuli ya Uzini.     
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Jamal Kassim Ali.wakati akiwasili viwanja vya Kampeni ya Jimbo la Uzini.  
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, akimtambulisha Mgombea wa CCM Jimbo la Uzini, Mohammed Raza, katika uzinduzi  uliofanyika katika Viwanja vya Skuli ya Uzini Wilaya ya Kati Unguja.     

 Mgombea wa CCM Jimbo la Uzini Mohammed Raza, akitowa sera za Chama chake katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni ya Jimbo hilo uliozinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume.   
 Wananchi na Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea wao alipokuwa jukwaani akitowa sera zake kwa Wananchi wa Jimbo hilo na kuomba Kura.katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni.  
 Baadhi wa Wanachama wa CCM walioingira katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi hiyo katika kura za maoni,kwa bahati kura zao hazikutosha wakimsikiliza Mgombea wa CCM Mohammed Raza akimwaga sera za Chama chake katika Mkutano wa Kampeni.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa, akitowa nasaha zake kwa Wanachama wa CCM wa Jimbo la Uzini katika Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni katika viwanja vya Skuli ya Uzini.  
 Katibu Mkuu wa CCM Mkama, akiwahutubia  Wanaccm wa Jimbo la Izinu katika Mkutano wa Kampeni.   
 Vijana wa CCM wakihamasisha katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni ya Jimbo la Uzini.
Baadhi ya Wanachama wa CCM, wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Dk. Amani Abeid Karume akizinduwa Mkutano wa Kampeni kwa Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Uzini, katika Uchaguzi Mdogo.  
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, akitowa maelezo ya Uzinduzi wa Kampeni ya Jimbo la Uzini. 
 Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohammed Seif Khatib, akiwahamasisha Wananchi wa Jimbo lake katika Mkutano wa Kampeni uiliofanyika katika Viwanja vya Skuli ya Uzini.  
 Wanachama wa CCM wakihamasisha Wananchi wa Jimbo la Uzini kukipigia kura cha cha Mapinduzi wakiwa na Bango.

 Msanii wa Kizazi Kipya IT,akiimba wimbo wa kumpigia kampeni mgombea wa CCM Mohammed Raza.


Viongozi wakisimama kwa Dakika moja kumuombea aliyekuwa Mwakilishi wa Jim,bo hilo Marehemu Mwalim Mussa, kabla kuaza kwa Uzinduzi huo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.