Mwenyekiti Mstaafu CCM Ali Hassan Mwinyi amewataka wananchi wa Jimbo la Uzini kutofanya makosa kumchagua Mgombea wowote wa Chama cha Upinzani badala yake wamchague Mgombea wa CCM Mohammed Raza Daramsi ambaye ndiye mgombea anayefaa kwa ajili ya maendeleo yao
Mwinyi ameyasema hayo katika kiwanja za Manzese Uzini wakati alipokuwa akifunga kampeni za CCM katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Jimbo hilo
Amesema Mohammed Raza ni Mpenda maendeleo na anayejali watu hivyo wananchi wa Uzini wana kila sababu za kumchagua Mgombea huyo wa CCM ambaye anawazidi sifa wagombea wote wa vyama vya upinzani
Ameongeza kuwa kama watamchagua Raza matatizo ambayo yanalikabili Jimbo la Uzini yatakuwa yamepata suluhisho la kudumu kutokana na dhamira ya dhati iliyojengeka katika nafsi ya Mgombea wao na Chama chao
Ameyataja matatizo ambayo yanalikabili Jimbo hilo kuwa ni pamoja na Maji Safi na Salama, Elimu na Afya na kudai kuwa yanaweza kupata suluhu iwapo Raza atachaguliwa
Mwinyi ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewasisitiza mamia ya wananchi hao waliohudhuria katika kampeni hizo kutekeleza ahadi ya Chama kwa kumchagua Raza kama ambavyo Uongozi wa CCM ulitekeleza ahadi ya wananchi hao kwa kumsimamisha mgombea huyo ambaye alikuwa chaguo lao
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Balozi Seif Idd amewataka wananchi hao kutochezea bahati waliyoipata ya kumchagua Raza kwani ni mtu mwenye upendo na kuwajali wanyonge.
Mjumbe huyo ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar amesema kuwa ikiwa Raza ameweza kusaidia wananchi wa Majimbo mbali mbali wakiwemo wa Jimbo lake hapana shaka Raza atakuwa na juhudi zaidi ya kuwasaidia wananchi wake mwenyewe
Kwa upande wake Raza amesema atahakikisha anawapatia maendeleo wananchi wa Jimbo la Uzini pale watakapomchagua na kuweza kuwa nao kwa bega katika kusimamia Ilani ya CCM
Amesema Ilani ya CCM ndiyo ilani ambayo inatekelezeka kwa maendeleo ya wananchi wa Jimbo hilo hivyo waendelee kumuunga mkono kwa kumpa kura ambazo zitamfanya awe Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ili awatumikie
Wananchi wa Jimbo la Uzini watapiga kura kesho kumchagua Mwakilishi wa Jimbo hilo ambapo jumla ya Wagombea Watano wa Vyama mbali mbali vya siasa nchini wanagombea nafasi hiyo iliyoachwa kufuatia kifo cha Mwakilishi wa Jimbo hilo.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar
Mzee mwinyi naona anatutisha, anasema wamchague Raza ili awawakilishe bungeni?
ReplyDeleteHivi kwani, kwa vile marehemu alikua pia mbunge anaewakilisha baraza la wawakilishi bungeni ni lazima Raza nae awe mbunge?..wadau nisaidieni hapa!
Namna bunge la sasa lilivyo, kwa kweli mimi sina imani na mbunge yeyote 'kilaza' hata kama ni wa chama changu.
Tuna yaona, kuna baadhi ya viongozi wetu hapa walikua mashujaa, baada ya kufika kule tunawaonea huruma, wanatetemeka na kukosea hata maneno ya kiswahili..kule sio mchezo!
Mzee Mwinyi acha kutubabaisha! Mimi sioni kwa uwakilishi wetu huu unavyotusaidia kuleta maendeleo kwenye majimbo yetu. Kwa Zanzibar yetu hii si wawakilishi wala si wabunge ambao wanatuletea mipango ya maendeleo au miradi ya maana zaidi ya kuazimishwa gari na mabusati na mbunge au mwakilishi kwa ajili ya shughuli za dharura badala ya miradi na mipangilio imara ya kuinua hali za wananchi.
ReplyDeleteHivi kama serikali kuu imeshindwa kuwaletea huduma hizi muhimu wananchi unategemea Raza atoe pesa zake mfukoni asuluhishe matatizo ya anaowawakilisha? Wewe Mzee Mwinyi umekuwa rais wa Zanzibar na Tanganyika vile vile, jee kwa nini hukuweza kuhakikisha kuwa Zanzibar kwa udogo wake huo inaondokana na kadhia hizi za uduni wa maisha unaopelekea wananchi wake kukosa mahitaji muhimu hata leo umtegemeshe Raza kwa wananchi wa jimbo la Uzini? Tuwe wakweli na wenye kufikiria tunachotaka kukisema kwanza kabla ya kukitamka badala yake kinakua hakileti maana.
Du..tena kweli!
ReplyDelete