Habari za Punde

SACCOS Zashauriwa Kufuata Taratibu za Usajili

Na Mwanajuma Mmanga

WIZARA ya Kazi, Uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika imewataka wananchi kufuata taratibu za usajili wa SACOS ili waweze kupatiwa mikopo na kujikwamua na umasikini nchini.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa ushirika wa kuweka na kukopa, Khamis Simba alipozungumza na mwandishi wa habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki.

Alisema SACCOS katika wilaya zote za Unguja na Pemba hutoa fursa na taaluma kwa wananchi kuhakikisha wanapata mikopo nafuu itakayowawezesha kuimarisha miradi yao katika kujiendeleza kimaisha .


Nae Katibu wa kikundi cha kuweka na kukopa cha Kinduni wilaya ya Kaskazini B Unguja alisema."

Kikundi chetu kina uhaba wa fedha kutokana na wanachama kuchelewesha michango, Katibu wa kikundi cha kuweka na kukopa wilaya ya Kaskazini 'B', alisema.

Alisema kikundi hicho kinahitaji kupatiwa mikopo kwa lengo la kukuza na kuendeleza shughuli zao ikiwemo chachu ya kuharakisha maendeleo ya kikundi hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.