BARAZA LA MADAKTARI – ZANZIBAR
SHERIA YA MADAKTARI NA MADAKTARI WA MENO, NO. 12 YA 1999
KWA MADAKTARI WOTE.
Madaktari wote wanaotaka kutoa na wanaotoa huduma Zanzibar (Medical and Dental Practitioners) wanatakiwa kujisajili kwa mujibu wa Sheria ya Madaktari na Madaktari wa Meno, chini ya kifungu cha 10(1) cha Sheria no. 12 ya 1999 . Madaktari wote wanatakiwa kupeleka maombi yao ya usajili kwa BARAZA LA MADAKTARI - ZANZIBAR liliopo Hospitali ya Mnazi Mmoja .
Ni kosa kisheria chini ya kifungu cha 22 cha sheria hiyo, kwa Daktari yoyote kutoa huduma ya udaktari( medicine, surgery or Dentistry) bila ya kusajiliwa na kupewa kibali na baraza hilo.
Baraza limo katika mchakato wa kutaka kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaotoa huduma ya udaktari bila ya kusajiliwa. Baraza linasisitiza kwa wale madaktari wazalendo waliopewa usajili wa muda wafike haraka kwenye Baraza kwa kupatiwa usajili wa kudumu.
Mrajis
Baraza la Madaktari
P.o.Box 236
Tel. 0775045519
Mnazi Mmoja – Hospital
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment